1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WUHAN: Rais Jacques Chirac wa Ufaransa aendelea za ziara yake nchini China

27 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCye

Rais wa Ufaransa Jacques Chirac, anaendelea na ziara yake rasmi nchini China. Rais Chirac amewataka viongozi wa viwanda nchini mwake wapanue ushirikiano wao na China, siku moja baada ya kushuhudia kusainiwa kwa mikataba ya mabilioni ya dola kati ya Ufaransa na China.

Hii leo alikuwa mjini Wuhan ambako ameweka jiwe la msingi katika jengo la kiwanda kipya cha kampuni za kutengeza magari za Ufaransa, Peugot na Citroen.

Nchini Ufaransa usalama umeimarishwa huku maadhimisho ya mwaka mmoja tangu nchi hiyo iliposhuhudia machafuko ya nchi nzima yakitarajiwa kufanyika.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, amewaamuru polisi wawe katika hali ya tahadhari. Aidha amesema polisi zaidi watapelekwa katika maeneo yanayokabiliwa na hatari ya kukumbwa na machafuko na njia za mabasi katika vitongoji vya mji wa Paris.