1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Xi na Biden wawasili San Francisco kwa mazungumzo muhimu

Sylvia Mwehozi
15 Novemba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa China Xi Jinping wamewasili San Francisco, kuelekea mkutano unaosubiriwa kwa hamu kati ya viongozi hao wa mataifa mawili yaliyo na uchumi mkubwa duniani.

https://p.dw.com/p/4YobA
Indonesien Bali G20-Gipfel | Treffen Xi Jinping, Präsident China & Joe Biden, Präsident USA
Picha: Saul Loeb/AFP/Getty Images

Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa China Xi Jinping wamewasili San Francisco, kuelekea mkutano unaosubiriwa kwa hamu kati ya viongozi hao wa mataifa mawili yaliyo na uchumi mkubwa duniani.

Biden na Xi watafanya mazungumzopembezoni mwa mkutano wa kilele wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa nchi za Asia na Pasifiki APEC jijini California unaoanza leo.

Marais hao wanakutana wakati kukiwa na ongezeko la mivutano ya kibiashara, vikwazo na suala la Taiwan. Kuelekea mazungumzo hayo, Biden amesema Marekani haitafuti kujitenga na China bali inataka kuimarisha mahusiano ya nchi hizo mbili yaliyodorora miaka ya hivi karibuni.

Mkutano wa kilele wa APEC unahudhuriwa na mataifa yapatayo 21 ambayo kwa pamoja yanachangia takriban asilimia 60 ya uchumi wa dunia. .