1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyoandikwa magazetini nchini Ujerumani

19 Oktoba 2006

Kesi dhidi ya Manfred Kanther yasikilizwa upya na kisa cha kuteswa Murat Kunarz ndizo mada zilizotangulizwa mbele na wahariri hii leo

https://p.dw.com/p/CHUf

Mada zilizohanikiza magazeti ya Ujerumani hii mleo ni pamoja na kufunguliwa upya kesi ya Manfred Kanther ya kashfa ya kukusanywa fedha kwa njia za udanganyifu na chama cha CDU katika jimbo la Hesse na kisa cha Murat Kunaz,mjerumani mwenyewe asili ya kituruki aliyeshikiliwa hadi agosti iliyopita katika kambi ya Marekani ya Guantanamo huko Cuba.

Tuanze lakini na kufunguliwa upya kesi ya Manfred Kanther.Korti kuu ya Ujerumani imebatilisha hukumu dhidi ya waziri huyo wa zamani wa mambo ya ndani kutokana na dosari za kisheria:Kifungo cha nje cha miezi 18 na faini ya yuro 25 elfu ndio adhabu aliyopewa kwa kuhamishia nchi za nje mamilioni ya fedha ya chama cha CDU katika jimbo la Hesse.Wahariri kadhaa wa magazeti ya humu nchini wamekosoa uamuzi huo.Na wa mwanzo ni wa gazeti la KIELER NACHRICHTEN anaehisi:

“Hata kama huo mtu anaweza kusema ni ufanisi japo si kamili kwa mwanasiasa huyo mkakamavu aliyestaafu.Lakini wakati huo huo ni pigo kubwa kwa chama cha CDU.Kwasababu kilitajari jinamizi la kashfa ya kukusanywa fedha kinyume na sheria ndo limeshatoweka.Kinyume kabisa ndio kinachoshuhudiwa.Kadhia yote itaanza kusikilizwa upya na korti ya jimbo huko Wiesbaden .Madhara yake kwa chama cha Christian Democratic Union hakuna anaeweza kuyakadiria kwa sasa.Kwasababu uwezekano ni mkubwa kwamba pengine mahakimu watataka kujua mchango gani ametoa waziri mkuu wa jimbo la Hesse Roland Koch katika kisa hicho cha kukusanywa fedha kinyume na sheria.

Gazeti la OFFENBURGER TAGEBLATT linaandika:

„Korti kuu imepitisha uamuzi uliowavunja moyo wananchi wengi waaminifu humu nchini.Kesi dhidi ya mkusanya fedha wa chama cha CDU,waziri wa zamani wa mambo ya ndani Manfred Kanther lazma lazma isikilizwe upya.Mwanzo mwanzo uamuzi huo mtu atahisi si mbaya.Kwasababu hukmu iliyotolewa baada ya rufaa katika korti ya jimbo mjini Wiesbaden ni aibu tupu.Kifungo cha nje cha mwaka mmoja na nusu alihukumiwa Kanther mwaka 2005 kwasababu alitumia vibaya yuro milioni kumi.Kanther angestahiki kulala jela,lakini amenusurika kutokana na hukumu ya korti kuu.“

Na mhariri wa Kölner Stadt Anzeiger anasema:

„Manfred Kanther anaweza kufurahia kwamba malipo yake ya uzeeni yamenusurika.Uamuzi wa korti kuu wa kubatilisha hukumu ya „kukosa uaminifu na kuigeuza kua kifungo cha nje cha miezi 18,haukumshangaza mtu.Sio tuu wakili wa Kanther,bali hata mwanasheria mkuu aligundua dosari kubwa za kisheria katika hukumu hiyo.Ni aibu kubwa hiyo kwa korti ya jimbo mjini Wiesbaden.Duru mpya ya kesi mojawapo kubwa kabisa ya kashfa ya kisiasa humu nchini-haitamshughulisha mtu yeyote yule hivi sasa.

Mada nyengine inamhusu mfungwa wa zamani wa Guantanamo Murat Murnaz.Wizara ya ulinzi inakanusha madai ya mjerumani huyo mwenye asili ya kituruki kwamba aliteswa na wanajeshji wa kikosi maalum cha kupambana na magaidi KSK.Ripoti ya kamisheni ya uchunguzi imekiri kwa njia moja au nyengine,palifanyika mazungumzo kati ya Kunaz na wanajeshi hao nchini Afghanistan.Wanahariri wa magazeti wanahisi hoja zinazoteklwa zinayumba yumba.

Gazeti la SAARBRÜCKER ZEITUNG kwa mfano linaandika:

„Yadhihirika kana kwamba watu wanajitahidi kwa dhati kuchunguza madai ya Kurnaz-Hata wizara ya ulinzi inabidi ichunguze vilivyo kadhia hiyo.Kwasababu kama sivyo, hadhi ya jeshi la shirikisho Bundeswehr inaweza kuingia doa.Kwasasa bado hakuna anaestahiki kutupiwa lawama .Lakini mara ngapi mapigano dhidi ya ugaidi,miaka ya nyuma, yamezusha visa ambavyo awali hakuna mtu yeyeote aliyeamini kama kweli vimetokea.Lakini ushahidi hakuna.Ila pengine kwamba kuna walakini katika kuwasiliana wanajeshi waliowekwa mahala fulani na uongozi wao.“