1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyoandikwa magazetini nchini Ujerumani

18 Oktoba 2006

Kurejea madarakani serikali ya muungano nchini Poland na umaskini nditzo mada zilizotawala magazeti ya Ujerumani hii leo

https://p.dw.com/p/CHUg

Upande wa upinzani nchini Poland umeshindwa na madai yake ya kuitishwa uchaguzi mkuu.Waziri mkuu wa kihafidhina KACZYNSKI amekubaliana na washirika wake wawili waendelee na serikali ya muungano.Mada hiyo imechambuliwa na wahariri wa magazeti ya ujerumani,sawa na mjadala unaoendelea kuhusu hali ya umaskini nchini Ujerumani.

Kwanza lakini hali nchini Poland.Na gazeti la THÜRINGER ALLGEMEINE linaandika:

„Mtu ambae wiki chache tuu zilizopita alitimuliwa kwasababu ya kuchochea fujo,kufumba na kufumbua amegeuka mwokozi wa serikali ya muungano.Ni sadiki ukipenda hiyo.Kile kinachoangaliwa kama mwanzo mpya,kinamfanya mtu aashirie muungano huo wa pande tatu hautadumu .“

Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE linahisi hilo ni pigo kwa waziri mkuu KACZYNSKI.Gazeti linaandika:

„Sasa naibu makamo waziri mkuu wa zamani Lepper amelazimisha kurejea kwake serikali, la sivyo wabunge wa chama chake wangeunga mkono bunge livunjwe.Kwa namna hiyo, “kuuokowa“ muungano mjini Warschau,limekua pigo ambalo waziri mkuu KACZYNSKI hatoweza kulisahau haraka hivyo.Ndugu wawili wa Kaczynski waliwaahidi waliowapigia kura,watapiga vita rushwa na mitindo ya „kusabilia“ masilahi ya Poland.Lakini dola walilotaka kuliimarisha limezidi kudhoofika kwasababu ya wao kung’ang’ania madaraka.“

Gazeti la BADISCHE NEUESTEN NACHRICHTEN linachamabua hali jumla namna ilivyo na kuandika:

„Tatizo kuu katika nchi zote changa za kidemokrasi katika ulaya ya mashariki ni ukosefu wa maadili.Ikiwa nchi haitawaliki,chaguzi mpya lazma ziitishwe ili kumaliza udhia.Kiongozi wa serikali akisema uwongo na kukiri hadharani,lazma ajiuzulu.Katika nchi za magharibi ,jambo hilo ni la kawaida tuu-mtu haihitaji kuuliza.Katika nchi za mashariki,watu wanafanya kila la kufanya mradi wanaendelea kuwepo madarakani.“

Hata gazeti la HANDELSBLATT la mjini Düsseldorf linazungumzia suala hilo na kujiuliza:

„Nchi gani hiyo ya Umoja wa Ulaya ambako waziri na makamo wa waziri mkuu wanang’olewa kwa aibu madarakani,halafu wiki chache tuu baadae wanakabidhiwa upya dhamana zao tena kwa kujifaharisha.?

Nchini Poland jambo hilo linawezekana,kama mfano wa ANDRZEJ LEPPER ulivyodhihirisha.Na sasa kiongozi huyo wa wakulima anaefuata siasa kali za mrengo wa kulia,amezidi kupata kichwa.Kurejea kwake serikalini ni sehemu ya mbinu za kisiasa za waziri mkuu JAROSLAW KACZYNSKI za kung’ang’ania madaraka,hata kama zitachafua hadhi ya Poland.“

Mada ya pili inahusu mjadala unaoendelea kuhusu umasikini nchini Ujerumani.

Gazeti la ESSLINGER ZEITUNG linahisi:

„Maajabu makubwa haya.Hofu zimezidi kufumba na kufumbua kwasababu wataalam wa wakfu wa FRIEDRICH-EBERT wanajishughulisha na suala la hali ya jamii nchini Ujerumani .Mjadala kuhusu umaskini umeanza upya.Utafiti wa taasisi hiyo mashuhuri inayoelemea upande wa chama cha SPD haustahiki kutiliwa shaka.Lakini kwamba jamii ishtuke kwasababu ya utafiti unaozungumzia hali tete ya maisha,hapo watu wanaweza kushuku.