1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyoandikwa na wahariri wa Ujerumani hii leo

Oummilkheir25 Januari 2007

Hutuba ya rais Bush na kashfa ya Katsav magazetini

https://p.dw.com/p/CHTt

Hotuba ya rais George W. Bush mbele ya baraza la Congress na kashfa inayomkumba rais Mosche Katzav wa Israel ndizo mada zilizohanikiza katika magazeti ya Ujerumani hii leo.

Kuhusu hotuba ya rais George W. Bush gazeti la LANDESZEITUNG LÜNEBURG limeandika:

„Marais wababe wanazungumzia hali ya taifa,na marais dhaifu wanazungumzia hali ya enzi yao namna ilivyo.Hajaiteterekea hata chembe dhamiri alizojiwekea „Vita dhidi ya ugaidi.“Ndio maana hakuu badilisha mkakati wake anaouangalia kua ni wajib nchini Irak.Upanga ndio njia ya kuleta demokrasia na utulivu katika nchi hiyo yenye mito miwili.Ushupavu wa Bush hautoi fursa ya ufumbuzi wa kidiplomasia katika eneo la mashariki ya kati.Hali inatisha kwa dola lenye maguvu kupita kiasi ulimwenguni.“

Gazeti la LANDSHUTER ZEITUNG/STRAUBINGER TAGBLATT lina maoni sawa na hayo.Gazeti linaandika:

„Kila kitu kinaashiria kwa hivyo kwamba miaka miwili ya mwisho ya Bush itakua ya shida na kusisimua pia.Watafanya nini wademokrats kumzuwia rais na kulazimisha mkondo mpya kuelekea Irak kabla ya uchaguzi ujao?Ana usemi gani hivi sasa mtoto huyo wa Texas kuweza kutekeleza mkakati huo wenye baadhi ya mambo mepya ndani yake?Itakua aibu kubwa kwa Marekani ikiwa ikulu ya Marekani italazimika kupimana nguvu na baraza la Congress.“

Kuhusu hali nchini Irak gazeti la mjini Rostock OSTSEE-ZEITUNG linahisi:

„Kiongozi mwenye maguvu kuliko wote ulimwenguni hana njia nyengine.Ikiwa sio kwa sabababu ya miswaada ya azimio iliyokwisha wasilishwa mbele ya baraza la wawakilishi na katika baraza la Senet,basi kwasababu ya ukosefu wa fedha.“

Gazeti la Neues Deutschland la mjini Berlin linasema Bush hakubadilisha msimamo wake.“Vita dhidi ya ugaidi“ vilivyolengwa miongoni mwa mengineyo kuhakikisha viwanda vya Marekani vinajipatia mali ghafi kwa bei ya chini-vinapanuliwa.Na kwa kua hakuna ushindi utakaotokana na vita,kwa hivyo panahitajika nishati mbadala.Majimbo na miji kadhaa ya Marekani imetangaza hatua kali dhidi ya matumizi yanayokithiri ya mafuta.Lakini Hatua hizo hazitoshi kukabiliana na kitisho cha mabadiliko ya hali ya hewa.

Mada nyengine magazetini hii leo ni kuhusu kishindo anachotiwa rais Mosche Katsav wa Israel kutokana na tuhuma za kuhusika na visa vya ubakaji.Mwenyewe anasema hatojiuzulu hadi mashtaka yatakapotumwa rasmi mahakamani dhidi yake.

Gazeti la SUTTGARTER ZEITUNG lakini linahisi:

„Malumbano dhidi ya rais yanaiathiri sana Israel.Kishindo cha vita vya Libnan hakijatulia bado, licha ya vigogo kadhaa wa kijeshi kung’oka madarakani.Hadi wakati huu Israel imekua ikiamini,adui wa kutoka nje ndie chanzo cha kuungana jamii,sasa lakini jamii yenyewe haiwaamini tena wanasiasa wao.Kwasababu kisa cha Katsav ni kimoja tuu katika orodha ndefu ya kashfa zinazofanywa na wanasiasa.“

Gazeti la mjini Düsseldorf HANDELSBLATT linaandika:

„Mwanasheria mkuu ana hakika,ana ushahidi wa kutosha kuweza kumfungulia mashtaka Mosche Katsav.Wabunge wengi wa Israel ,mamoja wanatoka chama gani,wanahisi hivyo hivyo.Isimaanishe lakini anatolewa hukmu kabla ya kukutikana na hatia.Lakini hapa suala kubwa linahusiana na hadhi na murwa wa mfumo mzima wa kisiasa na taifa zima la Israel.Hadhi hiyo imechujuka kutokana na kashfa za rushwa na visa vya udanganyifu katika daraja ya uongozi wa kisiasa.