1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyoandikwa na wahariri wa Ujerumani hii leo

24 Oktoba 2006

KUhamia ng'ambo wataalam na kitabu cha kumbukumbu cha kansela wa zamani ndizo mada kuu magazetini hii leo

https://p.dw.com/p/CHUd

Kuongezeka mno idadi ya wajerumani wanaohamia ng’ambo na kitabu cha kansela wa zamani Gerhard Schröder anaesimulia miaka saba ya utawala wake ni miongoni mwa mada zilizogubika kurasa za magazeti ya Ujerumani hii leo.

Idadi ya wajerumani wanaohamia nchi za nje imegonga kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu miaka 50 iliyopita:Watu laki moja na 45 elfu wameihama Ujerumani mwaka jana-limesikitika baraza la viwanda na biashara nchini Ujerumani.

Kuhusiana na tatizo hilo ,gazeti la “Die MÄRKISCHE ALLGEMEINE la mjini Postdam linaandika:

“Upungufu wa wataalam,hasara kwa makampuni-huo ndio usemi ulioenea.Wakulaumiwa ni wanasiasa, kodi na gharama zao zinazovuruga motisha .Hizo ndizo lawama zinazotolewa.Lakini yote yasemwayo si kweli.Kwasababu wa kulaumiwa mwanzo kabisa kwa kuhamia ng’ambo kwasababu za fedha wataalam wa kijerumani ni makampuni yenyewe.”

Gazeti la mjini Bayreuth la NORDBAYERISCHE KURIER linaahisi:

„Vijana wanakumbwa na shida kupata kazi.Kizazi kipya kiitwacho kizazi cha „mazowezi ya kazi“ kinakabiliana na shida za kila aina wanaposaka ajira.Mishahara ya chini kwa kazi ya ujuzi wa hali ya juu ndio mitindo iliyoko na hayo ndio yanayowasikitisha na kuwavunja moyo ,au hata kuwakatisha tamaa vijana.Umati wa watu wanaoachishwa kazi ni hali nyengine inayochangia pia kuvuruga matumaini ya vijana.“

Gazeti la ALLGEMEINE ZEITUNG la mjini Mainz linahisi:

„Kati ya wahamiaji wa leo,kuna wengi, tena wengi kweli kweli ambao ni vijana wenye ujuzi wa hali ya juu wanaoamua kuihama nchi ambayo ndio chanzo cha wao kuelimika,katika wakati ambao wangebidi kuonyesha imani na uadilifu kama shukurani zao kwa nchi yao.Lakini kwakua hakuna anaeweza kuwaandamana kisheria,kilichosalia ni kutaraji tuu watamlaani shetani.“

Gazeti linalosomwa na wengi mjini Cologne la Express linachambua:

“Kipi hatukuahidiwa na wanasiasa katika kipindi cha miaka iliyopita.Mengi yamehusiana na aina mpya ya uhuru na ahadi za neema.Hata mate hayajawahi kukauka,yaliyosemwa yamedhihirika kua maneno matupu.Fikra nzuri mara nyingi zinapuuzwa au kupotolewa kwasababu ya mivutano ya kisiasa.Na hiyo sio njia nzuri ya kurejesha imani na kuleta mustakbal mwema nchini Ujerumani.

Mada ya pili magazetini inahusu kuchapishwa kitabu cha kumbukumbu cha kansela wa zamani Gerhard Schröder.Kitabu hicho kimezusha mjadala mkali humu nchini.Gazeti la SÜDKURIER la mjini Konstanz linaandika:

“Mtu akichambua kwa dhati vifungu vilivyokwisha chapishwa magazetini vya kitabu hicho,hatakosea akisema hakuna haja ya kudurusu historia ya serikali ya muungano wa vyama vya SPD na walainzi wa mazingira.Schröder anazungumzia kile ambacho kila mmoja anakijua au angalao akikiashiria.

Kwamba Lafontaine,hamshughulishi,kwamba havutiwi na Angela Merkel,na badala yake anavutiwa sana na Vladimir Putin-hakuna asiyejua.Kipya ni zile lawama alizotoa dhidi ya wafuasi wa mrengo wa shoto wa chama cha SPD na wakuu wa vyama vya wafanyakazi.Na hapo kansela wa zamani hajakosea aliposema wao ndio sababu ya kushindwa kwake.