1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yaliyochambuliwa na wahariri wa Ujerumani hii leo

Oummilkheir10 Aprili 2007

Miaka minne tangu alipopinduliwa Sadam ndio mada iliyohanikiza magazetini hii leo nchini Ujerumani

https://p.dw.com/p/CHTI

Tuanze basi na hali nchini Irak,miaka minne baada ya kutimuliwa madarakani Sadam Hussein.Gazeti la Die Welt linaandika:

“Hakuna cha kutia moyo hata kidogo..Irak baada ya kutekwa, imegeuka machinjoni ,mahala ambako kila mmoja anapigania madaraka na kichaa cha kidini..Nchi inayoelekea kutumbukia katika janga la vita vya wenyewe kwa wenyewe-miaka minne baada ya kukombolewa.Ni kweli kabisa- kuna makosa yaliyofanyika.Hakuna mwenye picha ya Irak mpya, nchi iliyogawika sehemu tatu kijamii na kidini ,iliyolazimishwa kusalia nchi moja kwa mkono wa chuma wa Sadam Hussein.Kutokana na maandamano ya umma uliojaa hasira ,mtu anaweza kusubutu kusema kwamba mpango wa kuipanga upya Irak umeshindwa na unabidi uachiliwe mbali.Lakini kufanya hivyo itakua sawa na kuwahini,sio tuu maelfu ya watu waliopoteza maisha yao ,lakini pia wengineo walio hai ambao bado wanajipa matumaini.”

Mod:

Hayo ni matoni ya Die Welt.Gazeti la „Die Tageszeitung linahisi Marekani imezama moja kwa moja ndani ya matope ya Irak.Gazeti linaendelea kuandika:

„Watu wanajiuliza kipi chengine kitokee ili viongozi wa mjini Washington wajifunze kutokana na makosa waliyofanya.Kutuma wanajeshi zaidi ,kama rais George W. Bush anavyopanga kufanya na kushikilia mbinu za matumizi ya nguvu hakutasaidia kitu isipokua kuzidisha maafa.Ikiwa Marekani inataka kuepukana na aibu,basi haina budi isipokua kukubali imeshindwa na kutangaza haraka mpango unaoaminika wa kuwarejesha nyumbani wanajeshi wake.Hata kama hawatasema bayana lini wanapanga kuondoka..

Mod:

Hayo ni maoni ya gazeti la mjini Berlin Die TAGESZEITUNG.

Mada ya pili magazetini hii leo inahusu fikra ya waziri wa uchumi wa serikali kuu ya Ujerumani kutaka kodi za mapato zipunguzwe.Gazeti la mjini Bonn GENERAL-ANZEIGER linaandika:

„Kusema kweli waziri wa uchumi amefungamanisha pendekezo hilo na masharti. Kwanza-na hapa kilichokubaliwa ndo kimeshakubalika- lazma nakisi ya bajeti isawazishwe.Na kusema kweli ametumia werevu wa hali ya juu hapo.Kwasababu hadi bajeti itakaposawazishwa,hakutakua na hata mwanasiasa mmoja kati ya hawa tuwaonao hii leo,atakaekuwepo madarakani.Mnasema tupunguze kodi za mapato?Sadiki ukipenda linashadidia gazeti la General Anzeiger.

Mod:

Mada yetu ya tatu na ya mwisho magazetini hii leo inahusiana na kuadhimishwa mwaka mmoja tangu waziri mkuu wa jimbo la RHEINLAND-PFLAZ, Kurt Beck achaguliwe kua mwenyekiti wa chama cha Social Democratic SPD.Magazeti kadhaa yamejishughulisha na mada hiyo-kama lilivyofanya gazeti la Der TAGESPIEGEL la mjini Berlin:

„Mwaka mmoja bila ya MATTHIAS PLATZECK inamaanisha:Mwaka mmoja pamoja na Kurt Beck.Na inamaanisha miaka mia moja ya SPD-iliyonona.Kua na Beck kama mwenyekiti wa chama cha kale kabisa nchini Ujerumani ni sawa na kufanya matembezi ndani ya eneo la kati la Mainz.Na bila shaka kuna mengi ya kuvutia,kuna kanisa kuu na madirisha yake mazuri ajabu-lakini hakuna cha kusisimua hivyo.Kwamba Beck ndio anaeongoza serikali mjini humo-ni sawa-Lakini jee ni sawa pia panapohusika na siasa za shirikisho la jamhuri ya Ujerumani?“-Limemaliza kuandika Der Tagesspiegel.