1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON: Vikosi vyatumia nguvu kuzuia maandamano

29 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLh

Serikali nchini Myanmar imesema,hali ya utulivu imerejea nchini baada ya majeshi kudhibiti maandamano.Vikosi vya serikali vilitumia nguvu kubwa dhidi ya watawa na raia waliokuwa wakiandamana,kupinga utawala wa kijeshi.Kwa mujibu wa serikali,watu 9 waliuawa,lakini wanadiplomasia wa kimataifa wanasema,idadi ya vifo huenda ni kubwa zaidi.

Serikali ya Myanmar ambayo pia hujuklikana kama Burma,imeimarisha vikosi vyake mitaani na nyumba za watawa zimezingirwa na wanajeshi wenye silaha.