1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON:Mjumbe maalum wa UM kukutana na mkuu wa Junta nchini Myanmar

1 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBL8

Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa Ibrahim Gambari anatarajiwa kukutanana na mkuu wa kijeshi wa Myanmar Than Shwe katika jitihada za kusitisha operesheni dhidi ya waandamanaji wanaopinga utawala wa miaka 45 wa kijeshi nchini Myanmar.

Operesheni hiyo imesababisha umwagikaji damu na imeshutumiwa na nchi mbali mbali.

Mjumbe huyo maalum wa umoja wa mataifa anaelekea katika makao makuu ya shughuli za kiserikali mjini Naypyidaw ambako natarajiwa kukutana na mkuu huyo wa Junta Than Shwe.

Bwana Gambari amesisitiza umuhimu wa mazungumzo baina ya utawala wa kijeshi na wapinzani.

Awali bwana Gambari alifanya mazungumzo na mwanaharakati wa demokrasia anaezuiliwa bibi Aung San Suu Kyi.

Maandamano ya kupinga utawala wa kijeshi nchini Myanmar yamesababisha vifo vya takriban watu 13.

Watu kadhaa pia wamekamatwa na kuwekwa kizuizini.