1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON:Vyombo vya usalama vyatumia risasi za onyo dhidi ya waandamanaji

28 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLu

Walinda usalama nchini Miyanmar wamepambana na waandamanaji katika mji mkuu wa Yangon.

Polisi wamefyatua risasi za onyo na kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaopinga utawala wa kijeshi nchini Myanmar.

Awali vyombo vya usalama vilifunga nyumba tano kuu za watawa katika mji mkuu wa Yangon na kutangaza marufuku ya kukaribia eneo hilo.

Umoja wa nchi za ASEAN umelaani matumizi ya nguvu dhidi ya wapinzani na umeutaka utawala wa kijeshi ufanye juhudi za kutatua mgogoro huo kwa amani.

Mawasiliano makuu ya mtandao wa internet yamekatizwa nchini Myanmar na ingawa maafisa wa mawasiliano wanasema ni kwa sababu ya kuharibiwa waya zilizo chini ya maji, waandamanaji wanasema serikali imehusika kukatiza mawasiliano hayo ili kuzuia kupelekwa nje taarifa zaidi na picha za video zinazo onyesha operesheni za vikosi vya serikali dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali ya kijeshi.