1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YANGON:Wanaharakati watatu wakamatwa na serikali

14 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CG1U

Serikali ya kijeshi ya Myanmar imewakamata wanaharakati wengine watatu wanaopinga serikali huku mchunguzi wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa aliyeko nchini humo akisistiza kuwa hatua hiyo imesitishwa.Watu hao walikamatwa walipokuwa wakisambaza vikaratasi vinavyokosoa serikali katika soko la Mingalar mjini Yangon.Wanaharakati wengine wawili walikamatwa hapo jana wakati Paulo Sergio Pinheiro mjumbe wa kutetea haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa alipokutana na mawaziri kwenye mji mkuu wa Naypidaw.Mjumbe huyo anatarajiwa kufanya mazungumzo na mawaziri wa mambo ya kigeni na Kazi kabla kurejea mjini Yangon hapo kesho.Ibrahim Gambari ni mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini humo na anasema''Baada ya kushauriana nao Serikali tayari imefutilia mbali sheria ya kutotembea…..kuondoa majeshi barabarani….vilevile kuachia zaidi ya watu alfu mbili mia saba waliokamatwa wakati wa maandanamo ya kudai demokrasia… ''