1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yar'Adua afariki

Sekione Kitojo6 Mei 2010

Rais Umaru Mussa Yar'Adua wa Nigeria amefariki dunia. Kiongozi huyo amefariki akiwa katika makao yake rasmi mjini Abuja jana baada ya kuugua kwa miezi kadha.

https://p.dw.com/p/NFlz
Marehemu rais Umaru Yar'Adua aliyefariki dunia jana Jumatano mjini Abuja .Picha: picture alliance/dpa

Rais Umaru Yar'Adua wa Nigeria amefariki dunia. Kiongozi huyo alifariki katika makao yake rasmi mjini Abuja jana baada ya kuugua kwa miezi kadhaa. Kutokana na kifo chake, kaimu rais Jonathan Goodluck ameapishwa leo kuwa rais mpya.

Kifo cha rais Yar'Adua kilithibitishwa na ofisi yake mapema leo baada ya vyombo vya habari kukitangaza.

Msemaji wa kaimu rais alieleza katika taarifa fupi kwamba rais huyo alifariki kwenye makao yake rasmi ya mjini Abuja.

Rais huyo alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo yaliyomfanya apelekwe Saudi Arabia kwa ajili ya matibabu katika hospitali ya mjini Jeddah.Alitibiwa huko kwa muda wa miezi minne bila ya kupata afueni.

Alirejeshwa nchini Nigeria mnamo mwezi februari lakini hakuweza kutoka hadharani

Afya ya hayati Yar'adua ilikuwa dhaifu tokea mwanzoni , baada ya kuingia madarakani.

Katika tamko kaimu rais Goodluck Jonathan amesema kuwa watu wa Nigeria wameondokewa na lulu kutoka kwenye taji na hata mbingu zipo pamoja na taifa la Nigeria katika kuomboleza.

Naye katibu wa serikali kuu ya Nigeria Mahmoud Yayale Ahmedi amesema kifo cha rais Yar'dua ni msiba mkubwa.

Tunaungana na kila mwananchi mwema wa nigeria na kila mtu katika kuomboleza msiba huu mkubwa."

Rais Yar'adua aliingia a madarakani na ahadi yaorodha ndefu ya kuleta mageuzi.

Aliahidi kupamnbana na rushwa , kuleta mabadiliko katika mfumo wa utawala wenye mapungufu mengi.

Rais Yar'dua pia aliahidi kuleta mabadiliko katika mfumo wa uchaguzi.

Rais huyo alipiga hatua katika kuleta mageuzi kwenye mfumo wa benki.

Rais huyo pia alitoa mchango muhimu katika kuleta amani katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Niger.Alitoa msamaha kwa waasi wa jimbo hilo.

Lakini katika uand mwingine Yar 'adua alilaumiwa sana kwa kung'ang'ania madaraka japo alijua kwamba hakuwa na uwezo w a kutekeleza majukumu yake kama rais kutokana na kusumbuliwa na maradhi.Aliondoka nchini mnamo mwezi novemna mwaka jana ili kupata matibabu nchini Saudi Arabia.

Baada ya malalamiko makali bunge la Nigeria lilipitisha azimio na kumpa makamu wake,Goodluck Jonathan mamlaka ya kukaimu kama rais.

Viongozi wa dunia wametuma salamu za rambirambi kwa watu wa Nigeria. Rais Obama amesikitishwa na kifo cha Yar'dua na amemsifu kuwa mtu aliekuwa mwadilifu.

Rais Boni Yayi wa Benin amesema nchi yake imempoteza rafiki.

Rais Yardua aliefariki akiwa na umri wa miaka 58 atazikwa baadae leo katika jimbo lake la uzawa la Katsina kaskazini mwa Nigeria.

Mwandishi/Mtullya Abdu/AFPE/

Mhariri/Sekione Kitojo