1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Yemen yakabiliwa na hatari ya 'kuporomoka' zaidi

Jane Nyingi
31 Mei 2017

Umoja wa mataifa umeonya kwamba vita vya wenyewe kwa wenyewe huenda vikaliporomosha taifa la Yemen huku kitisho cha  njaa kikiendelea  kuongezeka na visa zaidi ya elfu 55 vya ugonjwa wa kipindupindu vikiripotiwa.

https://p.dw.com/p/2dtde
Yemen Sanaa - Menschenmengen bei Essensausgabe
Picha: Reuters/K. Abdullah

Katika kikao cha baraza  la Umoja huo naibu katibu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na misaada ya kibinadamu Stephen O Brien  alisema hali iliyoko sasa imesababishwa  na vitendo vya wapiganaji wanaomuunga mkono rais wa zamani na waasi wa kishia wa Houthi,.Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa watu millioni 17 wanahitaji msaada wa dharura wa chakula nchini Yemen  ikiwa ni pamoja na  wengine millioni 6.8 walio katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa. Taifa hilo  maskini la kiarabu, tangu Septemba mwaka 2014 limeandamwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya waasi wa  Houthi  kuuteka mji mkuu sanaa na kumwondoa madarakanai  rais Abed Rabbo  Mansour Hadi ambae serikali yake  ilikuwa tayari ikitambuliwa na jamii ya kimataifa.Naibu katibu Umoja wa Mataifa anayehusika na misaada ya kibinadamu Stephen O Brien  amesema ni swala la kuhuzunisha kuwa raia wa Yemen wanakabiliwa na magonjwa mbalimbali na wengine kufariki  huku ulimwengu ukitazama. “Hili si swala ambalo halikutazamiwa .Ni matokeo ya moja kwa moja  ya hatua za wahusika na wanaunga mkono mgogoro Yemen.Hayo yote pengine yametokana na tofauti  zilizopo  katika jamii ya kimataifa.alisema O'Brien.Mwezi Marchi  mwaka 2015,muungano  unaongozwa na saudi Arabia na  kuungwa mkono na Marekani  ulianzisha kampeini dhidi ya waasi wa Kihouthi  wanaomuunga mkono rais aliyepinduliwa Ali Abdullah Saleh, ili kusadia  kurejea serikali inayotambuliwa na jamii ya kimataifa ya Manosur Hadi.Tangu wakati huo waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na taifa la Iran wametimuliwa  katika maeneo mengi ya kusini mwa Yemen ,lakini bado wanaudhibiti mji mkuu  Sanaa na sehemu kubwa ya kaskazini. Mwakilishi wa Umoja wa mataifa  nchini Yemen Ismail Ould Cheikh Ahmed amesema  vurugu hasa  zinaendelea  sehemu mbalimbali  nchi humo,lakini zimeongezeka   pwani ya magharibi ambako vikosi vya serikali  vinajaribu kupiga hatua  kuelekea bandari ya Hodeida na pia mji wa Taiz.Kutokana na hali hiyo Naibu Katibu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na misaada ya kibinadamu Stephen O Brien ana ombi hili "Naziomba nchi wanachama kuhakikisha juhudi zote  zinafanywa  ili  kuiweka bandari ya Hodeidah wazi na undeshaji wake  kuendelea kama kawaida.Mashambulizi  dhidi ya bandari ya Hodeidah si kwa maslahi ya upande wowote , kwasababu moja kwa moja  yatawatumbukiza raia wa Yemen katika baa la njaa.alisema naibu katibu huyoKundi la mashirika 22 ya kimataifa ,na masharika mengine yanayotoa misaada ya kiutu nchini Yemn  yalitaka baraza la uslama laUmoja wa matifa  kuchukua hatua na  kumaliza mapigano hayo yaliyockua muda mrefu.

Jemen Militär starte Offensive gegen Houthi-Rebellen ARCHIV
Wapiganaji wa serikali wanaopambana na waasi wa KihouthiPicha: picture alliance/dpa/Str
Shiiten Jemen Houthis
Waasi wa Kihouthi wakionyesha silaha zaoPicha: picture-alliance/AP Photo/H.Mohammed

Mwandishi:Jane Nyingi
Mhariri:Yusuf Saumu