1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YEREVAN: Steinmeier asema suluhisho laweza kupatikana

21 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQ7

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, amesema anaamini suluhisho linaweza kupatikana katika mzozo baina ya Armenia na Azerbaijan kuhusu eneo linalozozaniwa la Nagorno Karabakh.

Eneo hilo, lililo na idadi kubwa ya Warmenia, lilisababisha vita vya miaka sita baina ya Armenia na Azerbaijan mnamo mwaka wa 1994.

Baada ya kufanya mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Armenia, Vardan Oskanjan, waziri Steinmeier alisema pande zote mbili zimepiga hatua katika mazungumzo ya amani.

Frank Walter Steinmeier alikamilisha ziara yake katika eneo la kusini mwa Caucasus, hapo jana ambayo ilimpeleka pia nchini Georgia na Abhazia.