1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

YOGYAKARTA:Ndege yadondoka na kuteketea visiwani Java

7 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLS

Ndege moja ya abiria ya Indonesia imedondoka na kuwaka moto ilipolazimika kutua kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa Yogyakarta kisiwani Java na kusababisha vifo vya watu 21 na kujeruhi wengine 110.Manusura hao walipata majeraha ya moto kulingana na mashahidi.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu wa Australia John Howard raia 10 wa nchi yake walikuwa safarini katika ndege hiyo.

Picha za video zilizonaswa na mpiga picha wa Kituo cha Seven cha televisheni cha Australia aliyenusurika,zinaonyesha namna abiria hao waliolowa damu walivyotia juhudi kukimbia.Mlipuko mkubwa ulitokea pale moto ulipofika katika tangi la mafuta na kuteketeza baadhi ya abiria waliokuwa wamelala chini.

Rais Susilo Bambang Yudhoyono wa Indonesia ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika na kumteua Waziri wa Usalama kujua chanzo cha ajali hiyo ikiwemo uwezekano wa sababu zisizo za kiufundi.Hii ni ajali ya pili mbaya ya ndege nchini Indonesia kutokea mwaka huu.