1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZACHARO: Mioto yaendelea kuwaka kwa siku ya nne

27 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVX

Mioto iliyozuka katika misitu nchini Ugiriki inaendelea kuwaka kwa siku ya nne hii leo.

Mioto takriban 89 inawaka katika sehemu mbalimbali ncini humo huku upepo mkali ukiongezea nguvu mioto hiyo na kukwamisha juhudi za wazima moto za kutaka kuizima.

Kufikia sasa mioto hiyo imewaua watu 61 nchini Ugiriki. Wakati huo huo, tetemeko la ardhi lenye kipimo cha 5.1 katika kipimo cha Richter limetokea katika eneo la magharibi mwa kisiwa cha Kefalonia nchini Ugiriki mapema leo.

Hakuna ripoti zozote zilizotolewa kuhusu majeruhi wala uharibifu uliosababishwa na tetemeko hilo.