1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zaidi ya wachimba mgodi 26 nchini China bado wamenasa

7 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CYYk

BEIJING:Zaidi ya wachimbaji 26 bado wamenaswa chini mgodi wa makaa ya mawe huko China kufuatia kupasuka kwa bomba la gesi hapo jana.

Katika tukio hilo lililotokea kaskazini mwa jimbo la Shanxi, wachimbaji 70 waliuawa ikiwa ni ajali mbaya kuikumba sekta ya migodi katika jimbo hilo.

Maafisa wanasema kuwa miili ya wachimbaji hao imeopolewa, huku juhudi za kuwakoa waliyonaswa chini mgodi huo zikiendelea.

Sekta ya migodi ya makaa ya mawe nchini China inaelezwa kuwa ya hatari kabisa duniani ikiwa na matukio mengi ya ajali ambapo katika kipindi cha kati ya mwezi January na Oktoba mwaka huu kiasi cha wachimbaji 3,069 walikufa kutokana na matukio takriban 2,000 ya ajali za migodi.