1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zambia yatimiza miaka 50 ya Uhuru

24 Oktoba 2014

Zambia inaadhimisha miaka 50 tangu kupata uhuru kutoka Uingereza leo(24.10.2014). Wazambia wako katika sherehe hizo kubwa na wanajisikia fahari kwa nchi yao , kuwa huru.

https://p.dw.com/p/1DbWe
Armut in Südafrika
Umasikini umekuwa mkubwa miongoni mwa Wazambia licha ya utajiri wa madiniPicha: picture-alliance/NTB scanpix

Kitu muhimu hata hivyo ni utulivu wa nchi yao hadi sasa ambapo , nchi hiyo haijashuhudia mizozo ya kisiasa na ina udhabiti wa kisiasa baada ya kubadilisha uongozi mara tano bila misukosuko ya kisiasa. Hata hivyo rais wa sasa wa Zambia Michael Sata hatakuwapo katika maadhimisho hayo baada ya kupelekwa nje ya nchi hiyo kwa matibabu.

Baada ya rais wa kwanza wa Zambia Kenneth Kaunda kuiongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka 27 kwa kutumia mfumo wa chama kimoja , mwaka 1991 yalifanyika mabadiliko ya kisiasa na kuanzisha mfumo wa vyama vingi , anasema Helmut Elischer wa ofisi ya wakfu wa FriedrichEbert iliyopo katika mji mkuu wa nchi hiyo Lusaka.

Präsident von Sambia Michael Chilufya Sata
Rais Michael Sata wa ZambiaPicha: picture-alliance/dpa

Miaka kumi baadaye , wakati rais wa wakati huo Frederick Jacob Titus Chiluba alipojaribu kubadilisha katiba , na kutaka kugombea wadhifa huo kwa kipindi kingine cha tatu , kuliundwa muungano wa vyama vya kijamii ili kuzuwia hatua hiyo.

Mabadiliko ya uongozi

Mabadiliko ya tatu ya kiongozi yalikamilika mwaka 2011. Katika uchaguzi ulioendeshwa kwa amani kabisa wananchi wa nchi hiyo walifikisha mwisho miaka 20 ya uongozi wa chama cha Movement for Multi-Party Democracy MMD, na mgombea wa chama cha upinzani Michael Sata kutoka chama cha Patriotic Front PF aliingia madarakani.

Kupferbergwerk in Sambia
Machimbo ya madini ya shaba nchini ZambiaPicha: picture-alliance/Bildagentur-online/Tips-Images

"Ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Zambia imefanikiwa katika baadhi ya masuala ya kisiasa. Baada ya miaka 27 ya uongozi wa chama kimoja chini ya Kaunda , imefanikiwa kuingia mwaka 1991 katika mfumo wa vyama vingi."

Kiuchumi Zambia imeweza kupata mafanikio , japo si makubwa hivyo. Kutokana na hazina kubwa ya madini ya shaba , nchi hiyo imeweza kupata ukuaji wa uchumi wa karibu asilimia 6 mara kwa mara.

Umasikini umekithiri

Licha ya kupata ukuaji huo wa uchumi, lakini mafanikio hayo yameshindwa kufika kwa wananchi ambapo umasikini ni wa kiwango cha juu kabisa. Kiasi cha asilimia 70 ya Wazambia wanaishi katika umasikini mkubwa. Kutokana na machimbo hayo ya madini ni makampuni makubwa ya kimataifa tu ambayo hufaidika.

Makampuni hayo makubwa huacha fedha kidogo sana nchini humo, anasema mtaalamu wa wakfu wa Friedrich Ebert Helmut Elischer.

Tazara Railway Sambia
Reli ya Uhuru, Reli ya Zambia Tanzania , TazaraPicha: cc-by-sa-Jon Harald Søby

"Serikali inajaribu kubadilisha utaratibu huu, kwamba makampuni makubwa katika sekta ya madini wanatoa fedha kidogo mno kwa nchi hiyo. Mapato ya kodi kutoka sekta ya madini ni madogo mno ukilinganisha na kile makampuni haya inachokipata."

Zambia inatumia kiasi cha asilimia 53 ya bajeti yake kwa mishahara , anasema waziri wa fedha Alexander Chikwanda. Asilimia 25 tu ndio inayotumika katika kupambana na umasikini, mipango ya maendeleo na masuala mengine.

Sambia Wahlsieger Präsident Michael Sata
Mshindi wa uchaguzi wa mwisho Zambia Michael SataPicha: AP

Hofu imewaingia hata hivyo Wazambia katika sherehe hizi za kutimiza ncxhi yao miaka 50 , wakati rais wao Michael Sata hatakuwapo kutokana na kuugua. Makamu wa rais wa Zambia Guy Scott amemwambia kaimu rais wa bunge la Zambia Edgar Lungu kuwa ataongoza sherehe za kuweka shada la mauaji katika mnara wa uhuru mjini Lusaka pamoja na shughuli nyingine ambazo angehudhuria rais Sata leo Oktoba 24.

Mwandishi: Sandner, Philipp / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri: Yusuf , Saumu