1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zambia yawafukuza Wachina 30 kwa wizi wa madini

Daniel Gakuba
7 Juni 2017

Wizara ya mambo ya nje ya China imesema kuwa raia wa nchi hiyo waliokuwa wakishikiliwa nchini Zambia kwa tuhuma za uchimbaji haramu wa madini wameachiwa na wako njiani kurejea nchini mwao.

https://p.dw.com/p/2eFig
Afrikareise chinesischer Außenminister Wang Yi in Lusaka
Picha: picture-alliance/Photoshot/P. Lijun

China ilikuwa imeilalamikia Zambia, ikisema hakuna ushahidi wa kutosha dhidi ya Wachina hao 31, miongoni mwao akiwemo mwanamke mwenye mimba na mgonjwa wa Malaria. 

Hata hivyo, idara ya uhamiaji ya Zambia ilikuwa imesisitiza kuwa Wachina hao watafukuzwa nchini Zambia.

China imewekeza kiasi cha dola bilioni moja katika sekta ya madini nchini Zambia, lakini Wachina wanachukiwa na Wazambia kwa tuuma za kuwanyanyasa na kuwalipa mishahara duni. 

Mwaka 2012, wafanyakazi walimuuwa msimamizi wao mmoja wa Kichina na kumjeruhi vibaya mwingine katika mzozo wa malipo kwenye mgodi wa makaa ya mawe.

Mwaka mmoja kabla, polisi ya Zambia ilikuwa imewatuhumu wasimamizi wa Kichina kwa jaribio la kuuwa, baada ya Wachina hao kufyatua risasi katika mzozo mwingine wa malipo.