1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZANUpf yaongoza uchaguzi Zimbabwe

1 Aprili 2008

Chama-tawala cha rais Mugabe (ZANUpf) kinaongoza kidogo katika uchaguzi wa Bunge .upinzani wadai ushindi.

https://p.dw.com/p/DYZV
Mwisho wa Mugabe hauonekani bado .Picha: picture-alliance/ dpa

Zaidi ya siku 2 tangu wazimbabwe kupiga kura ,Tume ya Uchaguzi mpaka sasa haikutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais ambao chama kikuu cha Upinzani cha Movement For Democratic Change (MDC) kinadai kimemshinda rais Robert Mugabe,anaetawala tangu uhuru 1980.

Ni matokeo ya viti vya Bunge ndio yanayoendelea kutangazwa na kwa muujibu wa matokeo hayo, chama-tawala cha ZANUpf cha rais Mugabe kinaongoza kidogo mbele ya kile cha MDC cha Bw.Morgan Tsvangirai.

►◄

Viti 110 kati ya vyote 210 vikiwa vimetangazwa hadi sasa, chama-tawala cha rais Mugabe ZANUpf kinaongoza kidogo kikiwa na viti 53 kwa viti 51 vya chama kikuu cha upinzani cha MDC.Chama kidogo cha MDC kilichotengana na kikubwa kikiongozwa na Arthur Mutambara kimejipatia viti 6.

Hii ni kwa muujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe (ZEC).

Mtindo wa konokono wa kutangaza matokeo ambao sababu yake Tume inadai kunatokana na shida za mipango, kumechangia shaka shaka kuwa Tume ya Uchaguzi na vyombo vyengine vinavyodhibitiwa na dola vinajaribu kupitisha wakati ili kufanya mizngwe .

Chama kikuu cha Upinzani MDC kinadai kutokana na makisio yake kutoka kura za vituo vya uchaguzi kote nchini,kunampa mtetezi wao wa wadhifa wa urais Morgan Tsvangirai na chama cha MDC ushindi ulio wazi -dhahiri-shahiri.

Hesabu nyengine iliotolewa na shirika la Zimbabwe lisilo la kiserikal pia limempa kiongozi wa upinzani Tsavangirai uongozi katika kiti cha urais akiwa amejipatia 49.2% ya kura zote dhidi ya 42% ya rais Mugabe na mtetezi 3 ,waziri wa zamani wa fedha aliejitenga na chama cha Mugabe-ZANUpf Bw.simba Makoni akiwa nafasi ya tatu kwa 8.2%

Kikundi hicho cha ukaguzi wa uchaguzi cha Zimbabwe wakati kinabashiri kwamba kiongozi wa upinzani Tsvangirai atashinda sehemu kubwa ya kura katika kinyan'ganyiro cha kiti cha rais, hatajipatia ushindi wa moja kwa moja ili kuepuka duru ya pili ya uchaguzi.

Bw.Tsvangirai amepanga kuwa na mkutano na waandishi habari hii leo.

Kwa upande mwengine, nchi 7 zanachama wa Umoja wa Ulaya na Marekani, zimeitaka Tume ya Uchaguzi nchini Zimbabwe kuharakisha matokeo ya uchaguzi.

Slovenia,mwenyekiti wa sasa wa UU pia imeitaka Tume kuharakisha kutangaza matokeo.

"Kufanya hivyo kutapunguza hatari ya kuzuka machafuko"-taariofa ya Umoja wa Ulaya imesema.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe George Chiweshe,ameelezea mwendo wa konokono wa kutangazwa matokeo unatokana na shida za kufanya wakati mmoja uchaguzi wa rais, Bunge na serikali za mitaa.

Ingawa upepo unampiga rais Mugabe alien'gan'gania madaraka tangu uhuru April,1980 miaka 28 iliopita,wachambuzi wanaamini hatan'gatuka na ataendelea kuidhibiti Zimbabwe akiungwamkono mna vyombo vya dola-jeshi na polisi-turufu ambayo itamuwezesha kutojali sauti za wapigakura na kujitangazia ushindi.

Marwick Khumalo-mwenyekiti wa kikundi cha wachunguzi kutoka PAN-AFRICAN PARLIAMENT ameungama kwamba uchaguzi wenyewe ulikua huru,bila maonevu na wa kuaminika.Halkadhalika, kikundi cha wachunguzi cha Afrika-Karibic na Pasifik (ACP) kimesema vivyo hivyo.