1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ZANZIBAR : Waislamu wahimizwa kutumia uzazi wa majira

14 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsq

Waislamu wa Afrika wametakiwa wende na wakati na kukubali kutumia mabadiliko ya teknolojia kwa sababu Uislamu kama dini ni kwa ajili nyakati zote na unaweza kutumiwa kwenda sambamba na mabadiliko ya dunia ya kisasa.

Waziri wa Utawala Bora wa Zanzibar Ramadhan Shabaan ametowa rai hiyo leo hii na kutolea mfano kwa haja ya kupambana na ongezeko kubwa la watu Barani Afrika na ulimwengu wa Kiislam ambako kunatishia malengo ya maendeleo.

Akizungumuza katika mkutano wa siku tatu ulioandaliwa na Mtandao wa Shirika la Kiislam la Afrika kwa ajili ya Idadi ya watu na Maendeleo amesema Waislamu wanatakiwa watumie uzazi wa mpango ili kuweza kufanikisha malengo yao ya maendeleo na kwamba Uislamu ni kwa ajili ya nyakati zote na nyakati zimebadilika.

Masheik kutoka nchi 35 za Kiafrika wanahudhuria mkutano huo wenye lengo la kuangalia masuala ya maendeleo barani Afrika kwa mtizamo wa Kiislam.