1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zawadi ya Nobel leo kwa Ahtisaari

9 Desemba 2008

Rais wa zamani wa finland anatunzwa leo rasmi zawadiyake ya Nobel ya amani.

https://p.dw.com/p/GCSD
AhtisaariPicha: AP

Leo, Rais wa zamani wa Finland-Marttti Ahtisaari anatunzwa rasmi zawadi ya Nobel ya amani katika sherehe rasmi itakayofanyika mjini Oslo,Norway.Ametunukiwa zawadi hiyo kwa juhudi zake za upatanishi katika mizozo mbali mbali.Kamati ya Nobel mjini Oslo, ilipitisha uamuzi wake kwa hoja kwamba Ahtisaari amechangia mno tena kwa miongo kadhaa kutatua migogoro :

Nani Martti Ahtisaari ?

Ilikua mwanzoni mwa mwezi wa Februari,2007 alipokuwa anatoa mpango wake mjini Belgrade uliokuja kuchukua jina lake-kwa ufumbuzi wa mgogoro wa Kosovo.Hapo aliulizwa na muandishi habari iwapo hakufikia kikomo cha kukata tamaa.jibu lake:

"Ah, unajua majira yajayo ya kianza nitafikia umri wa miaka 70.Ningekuwa nimekata tamaa basi kitambo ningekuwa nimepumzika kitini bukheri-mustarehe.Sikati tamaa haraka.Katibu mkuu wa UM amenipa jukumu na ninalitimiza.Wengine pia wanafanya kazi yao.Usitarajie kuwa nitakata tamaa.Mimi nimezaliwa mwenye tamaa.Ingekuwa si hivyo, zamani nisingekuwapo hapa."

Alisema Ahtisaari. Alipojaribu kuutatua ugomvi baina ya waserbia na waalbania wa Kosovo na kuwapatanisha ,matumaini ya bw.Ahtisaari yalikumbana na mtihani mkubwa.Kiasi cha mwaka mmoja na nusu, wajumbe wa pande hizo mbili wakijadiliana mjini Vienna,na Bw.Ahtisaari akiwasikiliza na akiwa mpatanishi akitoa mapendekezo yake binafsi.Lakini juhudi zote hizo mwishoe zilikwa za bure.

"Katika maisha yangu marefu, nimejifunza kuwa binadamu wanapozungumzia muwafaka,sana hudhani upande mwengine uridhie utakayo.Na mara hii hali si tofauti."

Mwishoe, Bw.Ahtisaari alianza kutafuta ufumbuzi binafsi wa mzozo wa Kosovo akijitwika dhamanya aliopewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.Ufumbuzi wake juu ya mzozo wa Kosovo ni uhuru wa jimbo hilo utakoalindwa na kusimamiwa na vikosi vya kimataifa pamoja na kulindwa mno kwa haki za wachache.

Kwa muujibu wa Bw.Ahtisaari, shabaha ya mpango huo ni kujenga msingi wa Kosovo ilioimara ambamo jamii zote na hasa waalbania,waserbia na wenginedo wanaishi kwa amani,kwa utu na wakiendesha hali bora za kiuchumi.

Lakini Baraza la Usalama la UM awali halikuudhinisha mpango wa Ahtisaari kwavile Urusi iliuwekea kura yake ya veto kuuzima .Hii ikaongoza hapo februari mwaka huu,kwa waalbania wa Kosovo kujitangazia uhuru na rais wa kwanza wa Jamhuri huru ya Kosovo akawa Hashim Thaci.

Thuci alinadai kwamba Kosovo imepiga hatua ya kihistoria."Tunatangaza uhuru wetu kwa muujibu wa mpango wa Bw.Ahtisaari." alisema Thaci.

Tangu kutoa tangazo hilo hakuna mengi yaliobadilika huko Kosovo.

Juni mwaka huu, katiba ya kosovo ikapitishwa na imefuata msingi wa mpango wa Bw.Ahtisaari.

Waserbia hatahivyo, wanaendelea kupinga uhuru wa kosovo na kuwekwa huko vikosi vya Umoja wa Ulaya kwa kadiri harakati zake hazikuamuliwa na azimio jipya la Umoja wa mataifa.Mgogoro halisi wa Kosovo kwahivyo, bado haukupatiwa ufumbuzi.Wanasiasa wa kiserbia huko Kosovo, wameitikia kutunzwa zawadi ya Amani ya Nobel Bw.Martti Ahtisaari na Kamati ya Nobel mjini Oslo,kwa hasira.