1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelaya ajipenyeza kwa siri kurudi Honduras .

Abdu Said Mtullya22 Septemba 2009

Manuel Zelaya arejea nchini kisirisiri,na serikali ya mpito yatangaza amri ya kutotoka nje.

https://p.dw.com/p/Jm1y
Manuel Zelaya ,rais aliepinduliwa amerudi tena nchini Honduras lakini safari hii kwa kujipenyeza kwa siri.Picha: AP

TEGUCIGALPA.

Rais aliepinduliwa nchini Honduras Manuel Zelaya amerejea nchini humo kisirisiri na ameomba  hifadhi  kwenye  ubalozi  wa Brazil  katika mji mkuu  wa  nchi  hiyo Tegucigalpa.

Zelaya alierejea  nchini jana anapigania kurudi  katika mamlaka kwa njia ya maandamano  na mgomo wa nchini kote.

Bwana  Zelaya mwenyewe amehakikisha kwamba hapatakuwa na  matumizi  ya nguvu na  ametoa mwito wa  kufanyika  mdahalo baina ya  matabaka yote ya  jamii nchini Honduras.

Wakati huo huo kiongozi wa kipindi cha mpito nchini  Honduras ameutaka  ubalozi  wa Brazil umtoe bwana  Zeleya  na umkabidhi kwa serikali.

Na habari kutoka New York zinasema  waziri wa mambo ya nje wa Marekani  Hillary Clinton  ametoa mwito juu ya kufanyika mazungumzo  ili kuepusha  umwagikaji damu nchini Honduras wakati  serikali  ya mpito  imetangataza  amri  ya  kutotoka nje na  pia imefunga uwanja  wa ndege.