1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Bibi Condoleeza Rice nchini Libya

5 Septemba 2008

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi Condoleeza Rice anatarajiwa kuwasili nchini Libya baadaye hii leo katika ziara ya kihistoria.

https://p.dw.com/p/FBto
Bibi Condoleeza Rice ziarani LibyaPicha: AP

Bi Rice anapanga kukutana na kiongozi wa Libya Muamer Gaddafi hatua inayolenga kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili baada ya jamii ya kimataifa kuitenga kwa muda mrefu.Itakumbukwa kuwa hii ni mara ya kwanza kwa Waziri wa mambo ya nje Marekani kufanya ziara nchini Libya katika kipindi cha miaka 55.Marekani imerejesha rasmi uhusiano na Libya ulisitishwa mwaka 1981 baada ya kuiweka kwenye orodha ya mataifa yanayofadhili ugaidi.

Ili kupata picha halisi Thelma Mwadzaya amezungumza na Suleiman Yussuf mwandishi wa habari aliye mjini Tripoli nchini Libya.