1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Gaddafi yashutumiwa vikali

10 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZhz

PARIS

Afisa wa ngazi ya juu wa haki za binaadamu nchini Ufaransa amemshutumu vikali kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi kabla ya kuanza ziara yake rasmi nchini Ufaransa leo hii kwa kusema kwamba Ufaransa sio kizulia cha kukanyagia mlangoni ambacho anaweza kukitumia kupangusia miguu iliorowa damu ya uhalifiu wake.

Waziri wa nchi katika masuala ya haki za binaadamu Rama Yade wa chama cha serikali ya mrengo wa kulia wa wastani amesema kwenye mahojiano na gazeti yaliochapishwa leo hii kwamba wakati wa kufanyika kwa ziara hii hususan ni mbaya kwamba anawasili katika Siku ya Haki za Binaadamu.

Ameliambia gazeti la kila siku la Parisian kwamba Ufaransa sio tu uwiano wa biashara na kwamba haipaswi tu kutia saini mikataba ya biashara na Gaddafi bali pia idai kupatiwa hakikisho juu ya haki za binaadamu nchini mwake wakati wa ziara yake hiyo ya siku tano.

Libya inatazamiwa kunuwa ndege aina ya airbus zenye thamani ya zaidi ya euro bilioni 3 pamoja na mtambo wa kuzalisha umeme kwa nguvu za nuklea na vipuri vya kijeshi.