1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Hillary Clinton mashariki ya Kati.

Munira Mohammed/ Reuters6 Machi 2009

Ziara ya kwanza ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton ilikuwa kutuliza hali tete Mashariki ya Kati, na kutoa sura mpya vipi utawala wa Barack Obama utaendesha shughuli Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/H72Y
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton alifanya ziara ya kwanya Masshariki ya KatiPicha: AP

Mkutano mjini Cairo nchini Misri wa kufuatilia ahadi iliyotolewa na jumuiya ya kimataifa kusaidia kujenga upya Gaza, ulitumiwa na mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa ya kiarabu wakiongozwa na Saudi Arabia,kujaribu kuishawishi Syria kukatiza uhusiano wake na Iran.


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton wakati wa ziara yake mashariki ya kati alionyesha kujitenga na sera za rais wa zamani George Bush baada ya kutangaza mjini Jerusalem kuwa atawatuma wajumbe wawili mjini Damascus nchini Syria kuanza upya mazungumzo na rais Bashar Al Assad.


Akijibu wasiwasi wa Israel kuhusu Iran, Bi Clinton alisema Iran iliyo na silaha za kinuklia si tishio tu kwa Israel bali swala hilo lilikuwa miongoni mwa agenda zake kuu wakati wa mkutano wa kilele wa viongozi wa mataifa ya kiarabu katika mji wa kitalii wa Sharm el Sheikh kuikoa gaza.


Duru za Israel zilimnukuu Bi Clinton akisema lengo la Marekani ni kuunda usalama wa pamoja wa eneo hilo kukabiliana na tishio la Iran la silaha za kinuklia.Bi Clinton aliahidi kuwa marekani itashauri na kushirikiana na Israel kuhusiana na mazungumzo ya baadaye na taifa la Iran.Waziri huyo wa mamabo ya nje wa Marekani alisisitiza kufungua mlango wa mazungumzo haimaniishi kukubaliana na mpango wa kinuklia wa Iran.


Iran kwa upande wake ilijaribu kuyashawishi mataifa ya eneo hilo kujitolea kuwaunga mkono Wapalestina katika harakati zao za kukabiliana na Israel.


Huku Hamas wakikaribisha hatua hiyo ya Iran katika ukiongo wa magharibi rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas pomoja na na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton wakati wa ziara yake mjini Ramallah, walichukua msimamo mkali dhidi ya kile alichokitaja majaribio ya Iran kujiingiza katika maswala ya Palestina.


Rais Abbas alisema badala ya kuisadia hatua hiyo itadhuru Palestina.Rais huyo alisema Iran imekuwa ikijaribu kuchochea mgawanyiko wa Wapalestina wakati hasa Hamas na chama cha Fatah wanafanya mazungumzo ya kuunda serikali ya umoja wa taifa.


Japokuwa mjini Jerusaleum Bi Clinton alitamka upya ungwaji mkono kikamilifu wa Israel na Marekani, akiwa Ramallah alionekana kukubaliana na wazo la kuundwa kwa dola mbili kama ilivyopendekeza utawala wa Palestina.


Wazo hilo la kuundwa kwa dola la Palestina limekuwa likipingwa vikali na waziri mkuu mteule nchini Israel Benjamin Nentayahu.


Wakati huo huo Clinton amedokeza kuwa huenda akaialika Iran kuhudhuria mkutano wa kimataifa mwishoni mwa mwezi huu nchini Afghanistan, katika harakati za kutoa sura mpya ya Marekani kukabiliana na mahasimu wake.


Clinton alisema ingawa Iran haijasema iwapo itakubali mualiko,Iran ina hamu kuu ya kujihusisha na kuwepo kwa taifa huru nchini Afghanistan, kwani wasiwasi wa Tehran kuzuia kuingizwa nchini mwao kwa madawa ya kulevya kutoka Afghanistan.











►◄