1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Muamar Kadhafi Roma.

11 Juni 2009

Kiongozi wa Libya aihusisha Marekani na ugaidi.

https://p.dw.com/p/I7br

Katika ziara yake ya kwanza nchini Itali,dola la zamani la kikoloni la nchi yake, Kiongozi wa Libya Muamar Kadhafi aliifungamanisha Marekani na Al Qaeda na kuituhumu kuiachia Iraq kugeuka nchi yenye " itikadi kali ya kiislamu."Muamar Kadhafi aliwaambia hayo wabunge wa Itali katika hotuba yake kali leo mjini Roma.

Akikumbusha hujuma ya mabomu ya Marekani nchini Libya,1968 iliouwa darzeni ya wakaazi pamoja nao mtoto wake wa kike , Kiongozi wa Libya, aliuliza:kuna tofauti gani baina ya hujuma za Marekani majumbani mwetu na vitendo vya kigaidi vya Al Qaeda ?Muamar Kadhafi, aliewasili Roma jana akitandikiwa busati jekundu la makaribisho makubwa nchini Itali alisema zaidi:

"Dunia inajikuta katika kivuli cha ugaidi wa dola rasmi....Osma Bin Laden hana dola,lakini Marekani ni dola."

Libya inapinga ugaidi alisema Kadhafi aliewasili Roma na ujumbe wa watu 200 kwa ziara ya siku 3 kwa shabaha ya kuimarisha mkataba wa urafiki uliotiwa saini mwaka jana.

Kiongozi wa Libya akaongeza "haitoshi kulaani ugaidi, inatupasa kuchunguza chanzo chake."

Muamar Kadhafi anaerejea katika jukwaa la siasa za kimataifa tangu kufuta mradi wake wa kuunda silaha za kuhilikisha umma 2003,alilalamika kwamba Libya haikupewa jaza kwa hatua yake hiyo.Liba kabla ilijitwika jukumu la ile hujuma ya 1988 ya ndege ya Pan Am juu ya anga la Lockerby,huko Schotland iliochukua maisha ya abiria 270 na ikalipa fidia ya dala bilioni 1.8 kwa jamaa wa wafiwa.

Kiongozi wa Libya amekuwa madarakani tangu kunyakua utawala 1969 na ameilaani Marekani kwa kuigeuza Irak pepo ya magaidi wa Al Qaeda.Magaidi hao,alisema Kadhafi hawangeweza kujipenyeza katika Irak chini ya uongozi wa saddam Hussein.Akasema kupitia m akosa ya Marekani ,Iraq imegeuka nchi yenye siasa kali ya kiislamu.Kadhafi akakariri matamshi aliotoa jana alipokumbusha madhambi yaliofanywa na itali wakati wa ukoloni nchini Libya akiwa pamoja na waziri-mkuu Silvio Berlusconi.

"Uhalifu mwingi ulipita enzi zile huku maalfu ya walibya wakiondoshwa nchini mwao."

Akigusia mkataba huo wa urafiki ambamo Itali itailipa Libya fidia yxa dala bilioni 5 mnamo robo-karne ijayo ,Kadhafi alisema,

"Hakuna fidia inayoweza kufidia kile Itali ya kikoloni iliowafanyia wananchi wa libya."

Kadhafi aliwsasili uwanja wa Ndege wa Roma akipita juu ya zulia jekundu la makaribishoo akiwa amevaa picha ya shujaa wa Libya alienyongwa kwa kubisha utawala wa kikoloni wa Itali. Picha hiyo aliovaa Kadhafi katika vazi lake inamuonesha Omar Al-Mokhtar alipokamatwa 1931 na uutawala wa kifashisti wa dikteta Mussolini.

Kilipozuka kitisho cha upande wa wabunge wa Upinzani kuigomea hotuba ya Kadhafi ya hii leo, viongozi wa Baraza la senate la itali waliamua kuhamishia kikao kutoka ukumbi mkuu kwenda ukumbi mdogo kidogo wa Zuccari.Ziara ya Kiongozi wa libya mjini Roma ilikosolewa mno na magazeti ya Itali.

Kadhafi hatahivyo, alimsifu waziri mkuu Berlusconi kwa kutia saini mkataba wa urafiki na Libya akitaja ni kitendo cha ujabari kuchukua hatua hiyo ya kihistoria kutaka radhi kwa umma wa Libya kwa Itali kuikalia kijeshi Libya kuanzia 1911 hadi 1947.Muamar Kadhafi,atahudhuria pia mkutano mwezi huu wa kundi la -G-8 -dola 8 tajiri,nchini Itali akiwa mwenyekiti wa UA.

Muandishi:Ramadhan Ali/AFPE

Mhariri:M.Abdul-Rahman