1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Papa Mashariki ya kati

Oumilkher Hamidou12 Mei 2009

Wahariri wanabishana kama ziara ya papa inatosha kuzawasisha suitafahamu

https://p.dw.com/p/HoSK
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani katika kumbusho la Jad VachemPicha: AP

Ziara ya Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni Mashariki ya kati, na mvutano katika serikali kuu ya muungano kuhusu mageuzi ya sheria za kupambana na maharamia wa kisomali,ndizo mada zilizochambuliwa zaidi na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.Tuanze lakini na ziara ya Papa Benedikt wa 16 katika jengo la makumbusho ya wahanga wa mauwaji ya halaiki ya Holocaust-Yad Vachem.Gazeti la DIE WELT linaandika:

Mjerumani asiyekua na asili ya kiyahudi, hawezi kuingia katika jengo hilo la makumbusho ya mamilioni ya wahanga wa utawala wa wanazi wa Ujerumani bila ya kua na moyo wa unyenyekevu.Na kwa papa huyo anaetokea Ujerumani hali ilikua hivyo hivyo.Katika hotuba yake,Papa ameonekana mara kwa mara akizungumzia juu ya mzizi wa pamoja kati ya wayahudi na wakristo,kama ilivyotajwa katika agano la kale,ili kushadidia umoja na sio mtengano kati yao.Kufuatia mfarakano uliosababishwa na kusamehewa na kurejeshwa katika umoja wa kanisa, muumini wa madhehebu ya Udugu wa Pius,Richard Williamson,anaebisha mauwaji ya halaiki-Holocaust ,ziara ya Papa inaangaliwa kua ni ya kusawazisha mambo.Hotuba yake imeaandaliwa kwa makini kupita kiasi kwa namna ambayo hakuna walakini unaoweza kutokea."

Gazeti la FRANKFURTER RUNDSCHAU linaandika:

"Nchini Jordan na nchini Israel,hakuwa na makuu hadi sasa,amejitokeza kwa hali ya tahadhari.Benedikt hakutamka neno lolote la kuudhi.Hiyo sio sababu lakini ya kumsifu kwasababu tahadhari mara nyingi inaonyesha hali ya mambo kijuu juu tuu.Mtu hahitaji kuwa msomi ili kuulaani mauwaji ya halaiki ya wayahudi Shoah,ni suala la maadili.Kuwanyoshea kidole na kuonya dhidi ya hisia za chuki dhidi ya wayahudi haitoshi,ikiwa kiongozi huyo wa kanisa katoliki ulimwenguni hatamki kwamba yeye mwenyewe ndie aliyemrejesha katika umoja wa kanisa katoliki,mbishi wa mauwaji ya halaiki ya Holocaust.

Gazeti la mjini Cologne,KÖLNISCHE ZEITUNG lina maoni mengine kabisa na linaandika:

Mara hii kila kitu anafanya vizuri.Papa Benedikt wa 16 ameingia mashariki ya kati kwa hekma na busara na kusawazisha baadhi ya suitafahamu zilizojitokeza miezi na hata miaka ya nyuma.Muhimu kuliko hotuba yoyote ile katika jengo la makumbusho la Jad Vachem ni ile namna Papa Benedikt wa 16 alivyoenekana kusononeka na yaliyotokea.Hotuba yake fupi imeondoa shaka shaka zilizokuwepo alipotamka: "Majina ya wahanga yasisahauliwe milele."Benedikt wa 16 ameitumia ziara yake kulaani aina yoyote ya ubaguzi wa kikabila na kidini na kuitolea mwito serikali ya mrengo wa kulia ya Israel izingatie umuhimu wa kuundwa taifa huru la wapalastina."

Schäuble stoppt GSG-9-Mission vor Somalia
Meli ya "Hansa Stavanger" ya Ujerumani iliyokua imetekwa nyara na maharamia wa kisomaliPicha: picture-alliance/ dpa

Mada ya mwisho magazetini hii leo inahusu mvutano katika serikali kuu ya muungano baada ya kusitishwa shughuli za kikosi maalum cha GSG 9 kinachopambana na maharamia karibu na fukwe za Somalia.Gazeti la PFORZHEIMER ZEITUNG linaandika:

"Mpango wa waziri wa mambo ya ndani Wolfgang Schäuble wa kufanyiwa marekebisho sheria ya kupambana na maharamia,mtu anaweza kusema hauna maana yoyote."Kwasababu sheria hiyo iliyopitishwa mwaka mmoja uliopita na bunge la shirikisho,tangu hapo inazungumzia juu ya kutumiwa nguvu ikilazimika ili kuwashinda nguvu maharamia.Ni dhahjiri kwamba Schäuble kwa kutaka sheria ifanyiwe marekebisho,alitaka kuitumia fursa iliyojitokeza tuu ili kutekeleza dhamiri zake za muda mrefu za kuzidisha nguvu za jeshi la shirikisho Bundeswehr,sio tuu baharini bali pia nchini.

Mwandishi :Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Abdul Rahman