1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya rais Erdogan Urusi

9 Agosti 2016

Rais wa Uturuki Recep Erdogan leo anatarajiwa kukutana na Rais Putin .Hiyo ni ziara ya kwanza ambayo Rais Erdogan anaifanya Urusi tangu ndege ya kivita ya nchi hiyo idung uliwe na majeshi ya Uturuki.

https://p.dw.com/p/1JeXI
Russland Recep Tayyip Erdogan und Wladimir Putin G-20 Türkei 2015
Picha: picture-alliance/AP Photo/L.Pitarakis

Ziara ya Rais Erdogan inaashiria kumalizika kwa mvutano baina ya Uturuki na Urusi uliosababishwa na hatua iliyochukuliwa na majeshi ya Uturuki ya kuitungua ndege ya kivita ya Urusi iliyodaiwa kuingia katika anga ya Uturuki kinyume cha sheria.

Mkasa huyo ulitokea mwezi Novemba mwaka uliopita.Kinachowashangaza wataalamu wa masuala ya kisiasa ni kasi ya kuondolewa kwa mvutano huo.

Rais Erdogan atakutana na mwenyeji wake Putin katika mji wa uzawa wa rais huyo, St.Petersburg. Hatua ya kuanza kuikaribia Urusi ilianza kuchukuliwa mwishoni mwa mwezi wa juni kwa barua iliyoandikwa kwa Rais Putin.

Chanzo cha mvutano kati ya Urusi na Uturuki

Kitendo cha majeshi ya Uturuki cha kuidungua ndege ya Urusi kilianzisha kipindi cha mvutano katika uhusiano baina ya nchi mbili hizo ambao hadi wakati huo ulikuwa wa ushirika wa ndani.

Urusi iliijibu hatua ya Uturuki kwa kupiga marufuku bidhaa za chakula za nchi hiyo kuingia nchini Urusi.Urusi pia ilisimamisha safari za ndege zake kwenda Uturuki sehemu inayopendwa sana na mamilioni ya watalii wa kirusi.Urusi pia ilisimamisha utelekezaji wa miradi miwili mikubwa : ujenzi wa bomba la gesi kupitia kupitia kwenye bahari ya Black Sea na kinu cha nyuklia.Marais Erdogan na Putin watatoa uamuzi juu ya miradi hiyo.

Türkei Syrien Kampfjet Russland Abschuss Grenzgebiet
Ndege ya Urusi yatibuliwa na jeshi la UturukiPicha: picture-alliance/dpa/Haberturk Tv Channel

Kasi ya hatua za kukaribiana tena baina ya Uturuki na Urusi ni ya kushangaza, hasa ikiwa mtu ataweza kukumbuka kauli kali zilizokuwa zinatolewa na kila upande hadi hivi karibuni tu.Ni kweli kwamba Rais Erdogan alisikitika juu ya kuangushwa kwa ndege ya Urusi, lakini alisema kuwa nchi yake haiwezi kuvumilia kukiukwa kwa mipaka yake.

Kabla ya kadhia ya ndege hiyo Uturuki mara kwa mara ilikuwa inalalamika juu ya kukiukwa anga yake na ndege za kivita za Urusi na hasa kwenye mpaka na Syria.

Wasi wasi ulikuwa mkubwa katika nchi za magharibi juu ya kutukia vita baina ya Urusi na Uturuki yaani mwanachama wa mfungamano wa kijeshi wa NATO

Rais Putin alilalamika kwamba Uturuki iliishambulia Urusi kinyemela.

Katika hotuba aliyoitoa mnamo mwezi wa Desemba mwaka uliopita Rais Putin alidai kwamba Uturiki ilikuwa inafanya biashara ya mafuta na magaidi wanaojiitadola la kiislamu.Televisheni ya Urusi pia ilikuwa inaendesha propaganda dhidi ya Rais Erdogan.

Mwanasiasa mwenye itikadi kali ya mrengo wa kulia nchini Urusi alifikia hatua ya kushauri kuishambulia Uturuki kwa silaha za nyuklia. Lakini tangu wiki za hivi karibuni ghadhabu imetulia nchini Urusi juu ya Uturuki. Siku chache tu baada ya barua yake kwa Putin, Rais Erdogan alianza kumpigia simu rais huyo wa Urusi.Zao la simu hizo ni makubaliano ya kukutana leo katika mji wa St.Petersburg.

Mwandishi:Goncharenko, Roman

Mfasiri:Mtullya Aabdu

Mhariri:Yusuf Saumu