1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Rais Karzai wa Afghanistan ,Marekani.

13 Mei 2010

Usuhuba kati ya Kabul na Washington

https://p.dw.com/p/NMm5
Karzai na Obama/Washington.Picha: AP

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan, anakamilisha leo ziara yake mjini Washington,Marekani , kwa mikutano na viongozi wa Congress-Bunge la Marekani pamoja na kutembelea makaburi ya wanajeshi wengi wa kimarekani, waliouwawa katika vita nchini Afghanistan.Ziara hii ya rais Karzai ,nchini Marekani ,ina shabaha ya kurekebisha usuhuba uliochafuka kati ya pande hizi mbili.

Wakati wa ziara hii ya siku 4 kuboresha uhusiano baada ya miezi kadhaa yapatashika kati ya pande hizo mbili,Rais Barack Obama, alisisitiza jana , kwamba, mvutano uliozuka kati ya serikali za Afghanistan na Marekani, umetiwa chumvi.

Rais Obama alisema,

"Jukumu letu ni kuona sisi na marafiki wa kweli na kuambiana ukweli wa mambo pamoja na rais Rais Karzai, upande gani tunapaswa kujitahidi zaidi.Jukumu la Rais Karzai ni kuiwakilisha nchi yake na kuona mamlaka yake yanahershimiwa."

KARZAI AJIZATITI

Rais Karzai nae alionesha kujizatiti kisiasa baada ya wiki kadhaa zilizopita kupaza sauti kupinga kujiingiza kwa nchi za nje katika mambo ya ndani ya Afghanistan.Ziara yake hii ya sasa huko Ikulu ya marekani imefanyika miaka 9 tangu hujuma ya septemba ilioichochea Marekani kuanzisha vita dhidi ya watalibani na Al Qaeda nchini Afghanistan na mpakani mwa Pakistan .

Rais Karzai, alimwambia mwenyeji wake Rais Obama " Tuko pamoja kati vita hivi dhidi ya ugaidi na kuna siku tumo furahani na kuna siku hatuko furahani."

Rais Karzai akaongeza,

"Kuambiana huko ukweli mambo kunaongeza tu kuimarisha zaidi ushirika wetu na kunachangia katika mafanikio tulionayo."

Ni wiki chache tu zilizopita itakumbukwa, wasaidizi wakubwa wa rais Obama walisema kwamba,madai ya rais Karzai kuwa wageni walianda njama za mizengwe katika uchaguzi uliopita Afghanistan , yalizusha wasi wasi mkubwa .Na hapo kabla, rais Obama alimwambia rais Karzai wakati wa ziara yake mjini Kabul,Afghanistan, kuwa alipaswa kuchukua hatua zaidi kupambana na rushua.

Lakini jana ,ilidhihirika, kila mmoja akinyunyiza maji katika moto ili kumtuliza shetani na Obama akasema amejionea kutengenea kwa hali ya mambo katika vita dhidi ya rushua,utawala bora na kazi bora ya kuandaa uchaguzi wa Bunge usio na mizengwe baadae mwaka huu.

OBAMA AUNGAMKONO :

Rais Obama, aliungamkono pia juhudi za rais Karzai za kuwashawishi wafuasi wa Taliban wanao yumbayumba kujumuika tena na jamii ya lakini kwa sharti kwamba, wanaachana mkono na Al-Qaeda na matumizi ya nguvu.

Afisa mmoja wa kijeshi wa Marekani, ambae hakutaka kutajwa, alisema rais Karzai alitaka kupatana mapatano ya usalama ambayo yangehakikisha kuwa Marekani inabakia kijeshi nchini mwake kupindukia Julai,mwaka ujao 2011 ambapo Marekani alitangaza itaanza kufunga virago kuondoka Afghanistan.

Mwandishi: Ramadhan Ali/ AFPE

Mhariri: Abdul-Rahman