1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ziara ya Wen Jiabao Ulaya

26 Juni 2011

Waziri mkuu wa China, Wen Jiabao, amewasili nchini Uingereza kutoka Hungary, katika ziara yake ya siku tano barani Ulaya.

https://p.dw.com/p/11jcg
Mgeni KaribuPicha: picture-alliance/dpa

Hii leo akifuatana na ujumbe wa mawaziri, waziri mkuu wa China, Wen Jiabao anatarajiwa kukutana na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron na waziri wa mambo ya nje nchini humo William Hague.

Wen Jiabao zu Besuch in Budapest Ungarn
Waziri mkuu wa China Wen JiabaoPicha: picture-alliance/dpa

Hapo jana Waziri mkuu Wen alitia saini makubaliano ya ushirikiano na waziri mkuu wa Hungary, Viktor Orban katika mji mkuu Budapest, ambacho kilikuwa ni kituo cha kwanza cha ziara yake hiyo. Waziri mkuu Wen alisema kuwa mzozo wa madeni Ulaya umeathiri uchumi duniani ukiwemo wa China. Aliongeza kuwa China ipo tayari kununua hisa za serikali ya Hungary na kutoa mkopo wa euro bilioni moja kwa nchi hiyo.

Wen aliwasili nchini Hungary ambayo inashikilia urais wa kubadilishana katika Umoja wa Ulaya, siku ya Ijumaa. Ni ziara yake ya pili barani Ulaya katika miezi tisa, na ni ziara ya kwanza ya kiongozi wa China nchini Hungary katika muda wa miaka 24.

Wen Jiabao zu Besuch in Budapest Ungarn
Wen Jiabao atoa hotuba HungaryPicha: picture-alliance/dpa

Hapo kesho anatarajiwa kuelekea mjini Berlin, Ujerumani. Kampuni za Ulaya zinatarajia uagizaji mkubwa kutoka China, lakini nyingi zinalalamika kuhusu ukosefu wa manufaa katika soko la China.

Mwandishi: Maryam Dodo Abdalla/alle
Mhariri:Kitojo Sekione