1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimbabwe haina fedha za unga wa mkate

2 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBTS

JOHANNESBERG:

Serikali ya Zimbabwe ya rais Robert Mugabe ilioishiwa na fedha haimudu sasa kulipia shehena ya tani 36.000 za unga ngano ilionasa katika bandari ya Beira ya nchi jirani ya Msumbiji.

Waziri wa usalama wa Zimbabwe Didymus Mutasa ameliambia gazeti rasmi la serikali litokalo jumapili-SUNDAY MAIL- kuwa upungufu wa fedha-taslimu una maana kwamba Zimbabwe haiwezi kugharimia shehena hiyo ya nafaka.

Aliahidi kwamba, serikali hatahivyo, inafanya juhudi kupata alao shehena itakayowawezesha wananchi kujipatia mkate.

Mkate umekua haba nchini Zimbabwe tangu serikali kuweka vikwazo juu ya bei za bidhaa zote na huduma mwishoni mwa mwezi wa juni katika shabaha ya kupambana na mfumko wa bei.