1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimbabwe-mshikamano usio faa

30 Machi 2007

Mzozo wa Zimbabwe utachukua muda zaidi kuumiza vichwa vya walimwengu.Mjini Dar-es-salaam,jana hakuna aliemkaripia wazi rais Mugabe.

https://p.dw.com/p/CB4z
Robert Mugabe
Robert MugabePicha: AP

Leo ijumaa, chama-tawala -ZANUpf-kinakutana kuamua iwapo rais Robert Mugabe, agombee tena wadhifa wa urais.

Ujerumani, ikiwa mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Ulaya, imeitisha uchunguzi maalumu juu ya kuteswa wapinzani na kukandamizwa uhuru wa kujieleza.Isitoshe, imetangaza wiki ijayo itashauriana kuiwekea Zimbabae vikwazo zaidi .

Kwa upande wake,serikali ya Afrika kusini,imepinga kujiingiza kwa aina hiyo katika maswali ya Zimbabwe .

Nchi jirani za Jumuiya ya (SADC) zilishindwa jana katika mkutano wao mjini Dar-es-salaam hata kuafikiana kumkosoa mwenzao wazi wazi. Je,Afrika inashindwa hata kutekeleza azimio lake binafsi la kuheshimu demokrasia na haki za binadamu ?

Ulipoasisiwa Umoja mpya wa Afrika (AU) miaka michache nyuma,ilihanikizwa na kupigwa upatu kuwa Afrika mpya, ya mageuzi ,demokrasia na yenye keheshimu haki za binadamu imezaliwa:

Ahadi tupu na maneno matamu hazitoshi.Katika swali la Zimbabwe, Afrika imeshindwa kutimiza ahadi zake.

Hii isieleweke dola kuu la kiuchumi- Afrika kusini ambalo liloutimua utawala wa kidikteta na wa kibaguzi miaka 15 tu nyuma ,laridhia Mugabe ayafanyao.Wazi lakini, atakae aweza kun’gamua kuwa hapa kuna mafungamano ya kihistoria.

Mugabe ni mkongwe wa vita vya ukombozi barani Afrika na kuna mafumngamano makubwa baina vigogo vinavyotawala Zimbabwe na Afrika Kusini.hatahivyo, historia isimtie mtu kitunga cha macho kutoona madhambi yanayopita Zimbabwe:

Kwani, katika milki ya Mugabe ya Zimbabwe,wapinzani wanakula mkomoto ,wanaandamwa na kukamatwa ovyo-ovyo.Waandishi habari, wanatiwa msukosuko,wakaazi wanahamishwa kwa nguvu kutoka sehemu moja na kupelekwa kwengine bila hiyari ipendapo serikali.

Rais Mugabe, yuko killeni mwa utawala wa mabavu usiojali ubinadamu.Na kinyume na madikteta wengine-mfano yule wa Belorussia, Lukaschenko, Mugabe, hafanyi lolote alao kuwatekelezea mahitaji ya lazima wananchi wa Zimbabwe.

Ni yeye mwenyewe alieigeuza nchi iliokua na neema ya kiuchumi na ghala ya nafaka na kugeuka nchi fukara ambamo umri wa wastani wa kuishi ni miaka 37 tu hivi sasa.

Afrika Kusini, haitaki kuikosoa Zimbabwe kwa hayo- alao si kwa kupaza sauti hadharani.

Nyuma ya pazia, inataka kupatanisha ili kuleta muafaka baina ya serikali na upinzani na labda, kumyakinishia mzee Mugabe mwenye umri wa miaka 83 kuwa sasa saa yako imegonga-yafaa kun’gatuka…

Upinzani nchini Zimbabwe, unahitaji kuungwamkono kutoka nje,kwani pekee ndani,hautamudu kukata pingu uliofungwa na udikteta wa Mugabe.

Swali hapa, si la kukomesha udikteta nchini Zimbabwe,bali kupata jibu la swali la kimsingi-iwapo Afrika jukumu lake ililojitwika- keheshimu haki za binadamu na demokrasia, sio tu imelibeba bali inalitekeleza.

”Afrika yafaa kuonahaya”-alisema askofu Desmond Tutu wa A.kusini –mshindi wa tunzo la nobel.Aliuliza “kitendeke nini tena Afrika mpaka tupaze sauti kukilaani ?Swali hilo hata baada ya kikao cha jana halikupatiwa jibu.