1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimbabwe yajipatia serikali mpya

Oumilkher Hamidou12 Februari 2009

Jee Tsvangirai atafanikiwa kweli kulazimisha msimamo wake serikalini?

https://p.dw.com/p/GsVr
Wazíri mkuu wa Zimbabwe Morgan TsvangiraiPicha: AP



Wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo wamemulika zaidi matokeo ya uchaguzi wa bunge nchini Israel,kuundwa serikali nchini Zimbabwe na kashfa ya kuchunguzwa data za watumishi wa shirika la usafiri wa reli la Ujerumani-Deutsche Bahn.Tuanzie Zimbabwe,ambako kiongozi wa upande wa upinzani Morgen Tsvangirai ameapishwa kuongoza serikali.Gazeti la TAGESZEITUNG linaandika:



"Mahasimu wawili wakubwa wanatawala pamoja.Baada ya miaka tisa ya mapambano ya kuania madaraka dhidi ya Robert Mugabe,Morgen Tsvangirai sasa amekabidhiwa wadhifa mpya wa waziri mkuu.Muimla aliyezeeka anasalia kileleni kama rais.Mpinzani wake,na mdogo wake wa karibu miaka 30,Tsvangirai,kiongozi wa "vuguvugu la mageuzi ya kidemokrasi" na mshindi wa uchaguzi wa bunge wa mwezi March mwaka jana,atabidi akazane sana akitataka msimamo wake ufuatwe katika serikali ya muungano.Kwamba serikali hiyo inaweza kushindwa,uwezekano huo haujaondolewa.Hata hivyo muungano huo unatoa fursa ya aina pekee ya kuiokoa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika."


Gazeti la BADISCHE NEUESTEN NACHRICHTEN linashuku na kuandika:


"Hata kama Tsvangirai ameiapishwa,haimaanishi kitu,anajikuta pale pale,katika mstari wa pili.Wizara zinazoongozwa na chama chake japo kama zinaonyesha kua ni muhimu,hata hivyo hazina madaraka ya kweli.Ya maana hapo ni wizara ya fedha tuu.Na wizara hiyo ni mtihani mkubwa hasa katika wakati huu ambapo uchumi wa Zimbabwe umeangamia.Zaidi ya hayo linazuka suala kama kweli Mugabe yuko tayari kushirikiana.Hata kama uamuzi wa kugawana madaraka ni wa kihistoria,haonyeshi lakini anataka kweli mageuzi.Mageuzi yanawezekana tuu ikiwa Mugabe atajitenga na siasa."


Hayo ni maoni ya gazeti la BADISCHE NEUSTEN NACHRICHTEN la mjini Karlsruhe.


Gazeti la FRANKFURTER ALGEMEINE linajishughulisha zaidi na kashfa ya data katika shirika la usafiri wa reli la Ujerumani-Deutsche Bahn na kuandika:


"Nani mwenye kuidhibiti hali ya mambo?Mradi  si wizara ya usafiri.Na wala si baraza la usimamizi ,kwasababu la sivyo wizara ya usafiri nayo pia ingearifiwa.Kamisheni maalum ya bunge la shirikisho-Bundestag itakua na kazi ngumu kuweza kugundua nani amefanya nini.Kamisheni hiyo lakini haiwezi kulinganishwa na mahakama ,na shirika la usafiri wa reli nalo pia haliwezi kulinganishwa na shirika la kibinafsi linalomilikiwa na wageni.Shirika hilo la usafiri lingestahiki kuonyesha hishma kubwa zaidi mbele ya baraza la kutunga sheria,lakini kumuachia mkaguzi ende likizo wakati kamisheni ya usimamizi inataka kumhoji,ilikua ni sawa na kulidharau bunge."


Gazeti la MÄRKISCHE ODERZEITUNG  linaandika:


Shirika la usafiri wa reli la Deutsche Bahn linachafua hata kile haba kilichosalia katika sifa zake za zamani.Ufafanuzi wa kina wa kadhia hii tuu ndio utakaoinusuru hadhi iliyochujuka ya shirika hilo linalomilikiwa na serikali.Kwasasa lakini hali ya mambo ni nyengine kabisa.Bado serikali iko nyuma ya mwenyekiti wa shirika hilo la usafiri wa reli -Deutsche Bahn,Mehdorn.Kansela Angela Merkel anataka kuepusha mfuasi wa chama cha SPD asikabidhiwe uongozi wa shirika hilo-Hata waziri wa usafiri Tiefensee anaweza kuzama katika bahari iliyochafuliwa na Mehdorn.Na yote haya yanajiri muda mfupi kabla ya uchaguzi mkuu.


Thelma.........Kwa hayo ndio...........