1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zimbabwe yalaumiwa na Shirika la Magazeti Duniani

Mutasa Omar7 Juni 2007

Shirika lenye kutetea haki ya magazeti Duniani (World Association of Newspapers) limelaani ukandamizaji wa vyombo vya habari nchini Zimbabwe,

https://p.dw.com/p/CHD3
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe
Rais Robert Mugabe wa ZimbabwePicha: AP

Shirika hili la kutetea uhuru wa magazeti (WAN) lenye makao yake mjini Paris Ufaransa, likiyawakilisha zaidi ya magazeti Elfu kumi na nane duniani, limeilaumu Govt ya Zimbabwe kuwakandamiza waandishi wa Habari ,kuwakamata ,kuwapiga, na kufuta vitambulisho vyao vya kufanyia kazi, yote hayo yanakwenda kinyume na sheria ya jumuia ya kimataifa, uhuru wa mtu kujieleza na pia kuwepo, uhuru wa vyombo vya Habari nchini Zimbabwe.

Shirika hili limeelezea visa kadha vilivyotokea nchini Zimbabwe, mfano, mwaandishi moja, Gift Phiri alikamatwa na kuteswa vibaya na Askari polisi wa Zimbabwe, kwa sababu ya repoti mbili alizo liandikia gazeti moja la Zimbabwe, lenye ofisi zake mjini London.

Mpiga picha moja akiwa na mwenzie walikamatwa na kupigwa na polisi walipokua wakijaribu kuripoti juu ya maandamano ya upande wa upinzani.

Msemaji wa Rais Mugabe ,George Charamba, akiwa pia katibu mkuu wa wizara ya Habari nchini Zimbabwe, amesema ripoti hio ya World Association of Newspapers, ni upuzi mtupu wala haina msingi wowote.

Nae Tafataona Mahoso, mwenyekiti wa Tume ya Habari ya Serekali, ilioanzishwa mwaka 2002 kutoa vibali kwa waandishi wa Habari amesema, baadhi ya waandishi wa Habari ni majasusi mfano, Edward Chikombo mwaandishi aliepiga picha kiongozi wa upinzani, Morgan Tsvangirai alipokua akiteswa na polisi.

Mwaandishi huyo hakua kwenye orodha ya waandishi waliosajiliwa kufanya kazi nchini Zimbabwe. Alisema Tafataona Mahoso. Mwaandishi huyo alikutikana baadae ameuwawa njee kidogo ya mji mku Harare.

Kufikia sasa Tume hio ya Habari ya Serekali nchini Zimbabwe, imeyafunga magazeti ma nne (4) yakujitegemea, huku ikiwakatalia kuwapa vibali waandishi wakujitegemea, na wale wakimataifa kufanya kazi nchini Zimbabwe.