1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zuma aapishwa.

Abdu Said Mtullya10 Mei 2009

Jacob Zuma aahidi kulinda haki za watu wote wa Afrika Kusini.

https://p.dw.com/p/Hn1E
Rais mpya wa Afrika Kusini Jacob Zuma ala kiapo.Picha: AP

PRETORIA.

Wiki mbili baada  ya  chama  chake cha ANC  kushinda  katika  uchaguzi mkuu, Jacob  Zuma  ameapishwa  kuwa rais mpya  wa Afrika Kusini.

Zuma  alikula kiapo mbele  ya maalfu  ya watu,   wananchi wa  Afrika  Kusini  na waalikwa  kutoka nje.

Rais huyo  wa nne tokea  kuondolewa mfumo wa  kibaguzi  nchini  Afrika Kusini  ametamka  kuwa  ana  wajibu wa kuendeleza malengo  ya  rais  wa awamu  ya  kwanza  ,Nelson Mandela.

Zuma  mwenye  umri  wa  miaka  67 amesema  daima   atatekeleza sera  zote zitakazoliendeleza  taifa  na   atayapinga yote yanayoweza  kuleta  madhara.

Rais huyo  mpya  pia ameahidi kulinda haki  za  wananchi  wote  wa  Afrika Kusini   na  amesisitiza  ulazima  wa umoja  wa  watu  wote, weusi na weupe katika  kutatua matatizo ya  kiuchumi na kijamii  yanayopaswa kushughulikiwa haraka.

ZA.