1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zuma kufikishwa mahakamani karibuni

20 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Ce9d

JOHANESBURG.Kaimu Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali nchini Afrika Kusini, amesema kuwa kuna ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani Kiongozi mpya wa Chama tawala nchini humo cha ANC Jacob Zuma kwa makosa ya rushwa.

Mwendesha Mashtaka huyo, Mokotedi Mpshe amesema kuwa uamuzi wa mwisho wa lini hatua hizo zitachukuliwa uko karibu.

Mashtaka hayo yanamuhusisha Zuma na kashfa ya ununuzi wa silaha ambao ulipelekea mmoja wa washauri wake kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.

Jacob Zuma hapo siku ya Jumanne wiki hii alichaguliwa kuwa kiongozi wa ANC baada ya kumshinda Rais Thabo Mbeki.Kwa kushinda nafasi hiyo Zuma amejiweka katika nafasi nzuri ya kuwa mrithi wa Rais Mbke katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2009.