1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zuma kupinga kurejeshwa mashitaka 783

Isaac Gamba
14 Septemba 2017

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma atakwenda mahakamani leo hii kupinga jaribio jipya la kutaka kurejeshwa kwa mashtaka 783 ya rushwa yanayohusiana na mikataba ya silaha ya 1990.

https://p.dw.com/p/2jxNi
Südafrika | Präsident Jacob Zuma
Picha: REUTERS/S. Hisham

Chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance (DA), kimekwenda mahakamani mara 11 tangu mwaka 2009 ili kushinikiza kufunguliwa mashitaka juu ya mikataba ya kijeshi iliyofikiwa baada kumalizika utawala wa ubaguzi wa rangi na utengano nchini Afrika Kusini ambayo yamemzonga Zuma kwa sehemu kubwa ya muda wake wa uongozi.

Mwaka 2005 aliyekuwa mshauri wa masuala ya fedha wa  rais Jacob Zuma Shabir Shaik alitiwa hatiani kwa kuwezesha utoaji wa hongo kwa kupatiwa mikataba hiyo na alihukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani.

Baadaye aliachiliwa kutokana na sababu za kiafya. Rais Zuma na maafisa wengine wa serikali yake walituhumiwa kupokea rushwa kutokana na manunuzi ya ndege za kivita zenye thamani ya dola bilioni 5 pamoja na boti za doria na silaha nyingine kutoka kwenye makampuni matano ya barani Ulaya.