1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANC yaelekea kwenye kudumisha theluthi mbili ya viti bungeni.

Abdu Said Mtullya24 Aprili 2009

Chama kinachotawala nchini Afrika Kusini kinaelekea kwenye ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/HcyF
Rais wa chama cha ANC Jacob Zuma.Picha: AP

JOHANNESBURG.

Chama cha ANC kinaelekea kwenye ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu nchini Afrika Kusini.

Wakati ni nusu tu ya kura zilizokwishahesabiwa, hadi sasa, ANC imeshafikia asilimia 67.3 Tume huru ya uchaguzi imethibitisha hayo.

Chama kipya cha upinzani Congress of the People hadi sasa kipo chini ya asilimia 8 wakati, chama kikuu cha upinzani Democratic Alliance kinachoongozwa na mwanasiasa wa kizungu, kimepata karibu asilimia 16 ya kura.

Wachunguzi wanasubiri kuona iwapo chama cha ANC kitafanikiwa tena kudumisha wingi wa theluthi mbili ya viti bungeni.

Wakati huo huo rais wa chama hicho Jacob Zuma anaetarajiwa kuwa rais wa nchi vilevile, ameshereherekea hatua ya ushindi iliyofikiwa na chama chake hadi sasa.Pamoja na maalfu ya washabiki wa chama chake , Zuma alinengua na kuimba mjini Johannesburg.

Matokeo kamili ya uchaguzi yanatarajiwa kufahamika baadae leo.