1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

10 wakatazwa kugombea urais Misri

15 Aprili 2012

Mbio za uchaguzi wa rais nchini Misri zimechukua sura nyingine baada ya mamlaka kuwaengua kwenye orodha ya wagombea vinara katika mchakato huo. Uamuzi huo umezusha kitisho cha hali ya usalama nchini humo.

https://p.dw.com/p/14e9e
Vinara kumi katika uchaguzi wa rais Misri wamekatazwa kugombea
Vinara kumi katika uchaguzi wa rais Misri wamekatazwa kugombeaPicha: Reuters

Miongoni mwa walioathirika ni aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi katika utawala wa Rais Hosni Mubarak, Omar Suleiman; mgombea wa kikundi cha Udugu wa Kiiislamu, Khairat al-Shater; na Muhubiri wa kisalafi Hazem Salah Abu Ismail ambaye mwanasheria wake alitoa onyo la kutokea kwa mgogoro mkubwa.

Omar Suleiman, mkuu wa zamani wa upelelezi wa Misri
Omar Suleiman, mkuu wa zamani wa upelelezi wa MisriPicha: dapd

Uchaguzi wa Rias ndio hatua ya mwisho kuelekea kwenye utawala wa kiraia, kutoka serikali ya mpito inayoongozwa na baraza la kijeshi lililochukua hatamu ya vigu vugu la maandamano yaliyomuondoa madarakani Rais Mubarak mwezi Februari mwaka 2011, baada ya kuiongoza Misri kwa zaidi ya miongo mitatu.

Newly released deputy Khairat al-Shater, mgombea wa kikundi cha udugu wa kiislamu
Khairat al-Shater, mgombea wa kikundi cha udugu wa kiislamuPicha: rtr

Wakuu wa majeshi nchini humo, wanatarajia kukabidhi madaraka kwa rais atakayechaguliwa Julai Mosi mwaka huu.

Hazem Salah Abu Ismail, mhubiri wa kisalafi
Hazem Salah Abu Ismail, mhubiri wa kisalafiPicha: picture-alliance/dpa

Kuenguliwa huko kwa wagombea hao, kunazidisha utata katika kipindi cha mpito cha kinachoambatana na machafuko na sasa nchi hiyo inapitia pia kwenye machungu ya chuki za kisiasa baina ya kundi la wanasiasa wanaoamini katika serikali ya kidini ambao awali walizuiliwa nchini humo na wanasiasa wanaounga mkono Rais Hosni Mubarak.

Masaa 48 ya kukata rufaa

Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini humo, Farouq Sultan, aliliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa jumla ya wagombea 10 kati ya 23 wameenguliwa kutoka kwenye orodha ya wagombea na wana muda wa saa 48 kukata rufaa.

Mmoja wa wagombea hao wa Hazem Salah Abu Ismail wa Salafi aliondolewa katika mchakato huo kwa kuwa mama yake ana uraia wa Marekani taarifa ambayo imetolewa na Shirika la Habari la Nchi hiyo SANA ambayo inatoa uhakika wa jambo hilo ambalo makundi ya kiislamu yamesema halina msingi.

Kitisho cha mgogoro

Nizar Ghorab, Mwanasheria wa Abu Ismail , anasema kuwa anatarajia mgogoro mkubwa kuibuka katika kipindi cha saa chache zijazo.

Naye mgombea kutoka kikundi cha Udugu wa Kiislamu Khaira al-Shater pia amekumbwa na fagio hilo la chuma la Jumamosi. Msemaji wake amesema kuwa wataupinga uamuzi huo.

Omar Suleiman ambaye alikuwa Mkuu wa Upelelezi katika serikali ya Rais Mubarak na Makamu wa Rais katika siku za mwisho za serikali hiyo naye pia amesema atakata rufaa kuhusu maamuzi hayo kwa mujibu wa msemaji wake.

Amr Moussa, miongoni mwa wagombea wanaopewa nafasi kubwa
Amr Moussa, miongoni mwa wagombea wanaopewa nafasi kubwaPicha: AP

Wagombea wengine wanaopewa nafasi kubwa ni Amr Moussa, Katibu Mkuu wa zamani wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Waziri wa Mambo ya Kigeni, pamoja na Abdul Moneim Abol Fotouh ambaye alifukuzwa katika kikundi cha Udugu wa Kiislamu mwaka uliopita baada ya kuamua kuendesha kampeni zake binafsi za uchaguzi wa urais.

Wengi kati ya wale walioenguliwa wameonesha upinzani dhidi ya hatua hiyo huku wengine wakidhamiria kuchukua hatua zaidi na baadhi wakinukuliwa kuwa uongozi uliofanya maamuzi hayo ujaindae kwa matokeo yake. Hali hiyo inazusha hofu ya usalama kwa nchi hiyo.

Mwandishi: Stumai George/RTRE

Mhariri:Daniel Gakuba