1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

43 wauawa na 80 wajeruhiwa na bomu Baghdad

1 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D167

BAGHDAD:

Idadi ya waliofariki kutokana na shambulio la bomu katika soko moja mjini Baghdad sasa imefika 46 na limewajeruhi wengine 80 . Polisi inasema kuwa shambulio hilo limefanywa na mwanamke mmoja ambae amejitolea mhanga kwa kujilipua.Mwanzo polisi ilikuwa imesema bomu hilo lilikuwa limefichwa katika kisanduku cha kuku.Lakini baadae ikasema limetokana na shambulio la kujitoa mhanga lililofanywa na mwanamkemmoja.Na katika tukio lingine, bomu lingine limelipuka katika soko ambalo nalo limekuwa limejaa na watu katika mji wa kusini wa Al-Jadida.Mlipuko huo umewauwa takriban watu 18 na kuwajeruhi kadhaa.