1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abbas na Mubarak kukutana.

27 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CyDY

Cairo.

Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas anatarajiwa kukutana na rais wa Misr Hosni Mubarak siku ya Jumatano kujadili mzozo wa mpaka kati ya Misr na eneo la Gaza.

Wakati huo huo watu wanazidi kuvuka katika eneo hilo la mpaka lililobomolewa kutoka kila upande.

Wapalestina wamevunja hali ya kuzingirwa na Israel kwa kubomoa kwa mabomu kuta za mpaka mapema wiki hii ili kuweza kupata mahitaji kutoka Misr.

Israel imesema wiki hii kuwa hatua ya kuizingira Gaza ni muhimu ili kujaribu kuzuwia makombora yanayofyatuliwa kuelekea Israel kutoka Gaza, eneo ambalo linadhibitiwa na chama cha Hamas. Akizungumza kuhusiana na suala hilo , mjumbe kwa ajili ya mashariki ya kati waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair ameonya kuhusu hatari ya mzozo wa Gaza kwa hatua za kuleta amani katika mashariki ya kati na ametoa wito kupatikana mkakati mpya kwa ajili ya eneo hilo.