1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABIDJAN: Rais Gbagbo kuhudhuria sherehe ya upatanisho

29 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBe4

Rais Laurent Gbagbo wa Ivory Coast siku ya Jumatatu,atatembelea makao makuu ya vikosi vya waasi wa zamani-FN katika mji wa Bouake.Hiyo itakuwa ziara yake ya kwanza katika eneo hilo, tangu uasi wa mwaka 2002,uliotaka kumpindua, kusababisha nchi hiyo kugawika sehemu mbili.

Gbagbo atasimamia sherehe itakayoashiria kusalimisha silaha.Hiyo pia ni sherehe ya upatanisho kufuatia makabaliano mapya ya amani kati ya Gbagbo na FN.Mkataba huo wa amani umepatikana chini ya usimamizi wa Burkina Faso.