1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA: Rais mpya ameapishwa nchini Nigeria

29 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwx

Umaru Yar’Adua ameapishwa kama rais mpya wa Nigeria.Katika sherehe iliyofanywa mji mkuu Abuja,Yar’Adua alipokea wadhifa wa urais akimrithi Olusegun Obasanjo anaeondoka madarakani.Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Nigeria kwa viongozi wa kiraia kupokezana madaraka.Yar’Adua ameahidi kuendelea na mradi wa maageuzi ulioanzishwa na Obasanjo.Makundi ya upinzani yameshutumu kuwa uchaguzi wa mwezi uliopita ulifanyiwa udanganyifu na wasimamizi wa kimataifa wamesema,uchaguzi huo si wa kuaminika.