1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABUJA.Spika wa bunge la wawakilishi Nigeria ajiuzulu kufuatia tuhuma za ruswa

31 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7BH

Spika wa bunge la wawakilishi nchini Nigeria Patricia Etteh amejiuzulu kufuatia shinikizo za wiki kadhaa za kumtaka ajiondoa kutokana na tuhuma za kuhusika na ulaji rushwa.

Patricia anadaiwa kuhusika na ufujaji wa dolla millioni 5 fedha za serikali kwa kuzitumia kununua magari 12 na kukarabati nyumba anayoishi pamoja na ya naibu wake ambazo ni mali ya serikali.Tume maalum iliyoteuliwa kuchunguza madai hayo imemkuta na hatia ya ulaji rushwa bibi Patricia ambaye ni kutoka upande wa chama tawala.

Kwa muda wa wiki kadhaa Spika huyo alikuwa amekataa kujiuzulu na kumpisha spika wa muda kuongoza mjadala kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Sakata hiyo imemtia aibu kubwa rais Umaru YarAdua ambaye aliahidi kutotoa nafasi kwa walaji rushwa lakini akashindwa kuingilia kati kesi hii licha ya upinzani mkali.