1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACAPULCO :polisi waingia mtegoni na kuuawa nchini Mexiko

7 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCUP

Watu wanane waliokuwa na silaha wamewaua polisi saba kwenye vituo viwili vya polisi katika mji maarufu wa Acapulco nchini Mexico. Washambuliaji hao walikuwa wamevaa sare za jeshi. Walienda kwenye vituo hivyo na kujitambulisha kuwa ni wanajeshi waliokuwa wanakugua silaha.

Polisi kwenye vitu hivyo walisalimisha silaha zao kwa hiari , na ndipo walipoanza kushambuliwa.