1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACCRA:Steinmeir amaliza ziara ya afrika

4 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcG

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier amemaliza ziara yake ya siku tatu barani afrika, ambapo kabla hajaondoka mjini Accra Ghana alisema kuwa ana imani ya kwamba mkutano kati ya wakuu wa Afrika na wa Ulaya utafanyika.

Mkutano huo umepangwa kufanyika mwisho wa mwaka huu nchini Ureno, ambapo hata hivyo kumekuwa na shakashaka ya kushindwa kufanyika kama ilivyokuwa miaka saba iliyopita.

Suala la kuhudhuria kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ndiyo kikwazo cha kufanyika kwa mkutano huo.Nchi za Ulaya zimemwekea vikwazo vya kusafiri Mugabe, ambapo viongozi wa Afrika wamesema kuwa kiongozi huyo ni lazima ashiriki vinginevyo nao hawatohudhuria.

Waziri Steimeir pia alielezea matumaini yake ya kufikiwa kwa suluhu la mzozo wa Darfur.