1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACMilan na Boca juniors finali

13 Desemba 2007

Finali ya kombe la klabu bingwa duniani,itakua kati ya Boca Juniors ya Argentina na AC Milan ya Itali.

https://p.dw.com/p/CbKk

Katika kombe la dunia la klabu bingwa mjini Yokohama,Japan, mabingwa wa Ulaya AC Milan waliikomea Urawa Reds ya japan bao 1:0 na kukata tiketi yao ya finali ya kombe hili dhidi ya mabingwa wa Amerika Kusini, Boca Juniors ya Argentina.

Olympic Lyon ya Ufaransa na Fenerbahce ya uturuki zimenyakua nafasi 2 za mwisho jana kwa duru ijayo ya champions league-kombe la klabu bingwa barani Ulaya.Wakati schalke imebakia timu pekee ya Ujerumani katika duru hiyo ijayo, mabingwa wa Ujerumani stuttgart waliaga jana mashindano.

Stadi wa timu ya taifa ya Mali, Frederic Kanoute achangia kitita cha euro nusu milioni kuokoa msikiti usifungwe mjini Seville,huko Spain anakocheza dimba.

Katika kombe la dunia la klabu bingwa nchini japan,mholanzi Clarence Seedorf amewapelekea salamu boca Juniors wa Argentina kwamba wachunge sawa sawa pale AC milan na Boca zitakapokutana kwa finali ya kombe hilo la dunia la klabu bingwa jumapili hii ijayo. Huo utakua mpambano wa marudio wa finali ya kombe la Toyota ya mwaka 2003.

AC Milan iliichapa leo Urawa Reds ya Japan-shukurani kwa bao la Seedorf mnamo dakika ya 68 ya mchezo.

Ili kuingia finali hiyo, Boca Juniors ya Argentina iliwatoa mabingwa wa Afrika Etoile du sahel ya Tunesia pia kwa bao 1:0 hapo jana.

Mashabiki 67,000 walisheheni katika uwanja wa Yokohama kuwaangalia Urawa Reds wakioewa darasa la dimba na akina kaka na Seedorf.

Uwanja wa Yokohama ni ule ule uliochezewa finali ya kombe la dunia la mataifa 2002 pale Brazil ilipotoroka na kombe hadi rio.

Katika changamoto za kombe la klabu bingwa

Barabi Ulaya-champions League tiketi 2 za mwisho kwa duru ijayo zilinyakuliwa jana-moja ikenda Ufaransa kwa Olympique Lyon na ya pili ikmalizikia Uturuki kwa Fenerbahce.

Mabingwa wa Ujerumani stuttgart wamepigwa kumbo kabisa msimu huu .Ni Schalke pekee iliobaki kupepea bendera ya Bundesliga katika champions League huku klabu za Itali na Uingereza zikitamba duru ijayo yarobo finali.

Wakati Lyon iliitia adabu Galsgow Rangers ya Scotland , Fenerbahce ilitoa CSKA Moscow.Manchester United ilitosha kutoka suluhu bao 1:1 na Roma kuingia duru ijayo.

Bayern Munich –viongozi wa Bundesliga-ligi ya Ujerumani wakati huu wanabidi mwishoni mwa wiki hii kuteremka uwanjani bila ya kipa wao Oliver Kahn watakapowatembelea Hertha Berlin jumamosi.Kocha Ottmar Hitzfeld amempiga faini ya dala 36,720 na kifungo cha mechi moja nahodha wake na kipa .hii inafuatia Kahn kuwakosoa wachezaji wenzake 2 na kuondoka katika sherehe ya x-masi mapema kabla kumalizika.

Munich inaongoza orodha ya Ligi kwa pointi 2 na ushindi huko berlin jumamosi utawapa usingizi mzuri wakati wa siku kuu za x-masi na mwaka mpya.Kwani, huo utakuwa mpambano wao wa mwisho wa Ligi mwaka huu.

Stadi wa timu ya taifa ya Mali na jogoo la klabu ya Seville ya Spain, Frederick Kanoute, ameuokoa msikiti mjini Seville, Spain usifungwe kwa kuuchangia Euro zaidi ya nusu milioni.Kanoute alitoa sadaka ya Euro 510,860 ili kuwawezesha waislamu wenzake huko Seville,Spain wasijikute hawana msikiti wa kwenda kusali.

Kanoute anaeichezea klabu ya huko ya Sevilla na akiongoza muda mrefu kwa kutia mabao akiichezea zamani mabibngwa wa Ufaransa Lyon.huu si mchango wake wa kwanza ,kwani ameanzisha wakfu nchini kwao Mali kuwasaidia watoto na hasa mayatima.

Halmashauri kuu ya Olimpik Ulimwenguni-IOC- jana ilimvua kabisa medali zote 5 malkia wa olimpik wa mbio fupi,muamerika Marion Jones.Jones alinyakua medali hizo katika michezo ya Olimpik ya Sydney,Australia, mwaka 2000.Tatu kati ya hizo zilikua za dhahabu.Jones ameungama kwamba alitumia madawa kutunisha misuli na kuongeza kasi-doping.