1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Alama za risasi kwenye magari ya kundi lililotoweka

6 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCLx

Tume ya wanadiplomasia wa Uingereza imewasili katika eneo la ndani la kaskazini-mashariki ya Ethiopia,ambako inadhaniwa kuwa Waingereza 5 walitekwa nyara.Ripoti zinasema kuwa magari matatu yaliotumiwa na kundi lililotoweka yamekutikana katika eneo hilo.Inasemekana kuwa magari hayo yana alama za risasi na mripuko. Miongoni mwa watu waliotoweka ni wafanya kazi wa ubalozi wa Uingereza katika mji mkuu wa Ethiopia,Addis Ababa.Kundi hilo la Waingereza 5 na Waethiopia 13 lilitoweka siku ya Alkhamisi katika jangwa la Afar.Siku ya Jumamosi,watano kutoka Waethiopia 13 walipatikana wakiwa wazima, karibu na mpaka wa Eritrea,nchi inayotuhumiwa kuhusika na utekaji nyara huo.