1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Ethiopia yakaribisha milenia mpya

12 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQX

Ethiopia hii leo imekaribisha milenia ya tatu kwa shangwe kubwa,ikiwa ni miaka saba baada ya ulimwengu mzima kuingia katika millenia mpya. Waziri Mkuu wa Ethiopia,Meles Zenawi amesema,ni matumaini yake kuwa milenia mpya itakuwa enzi mpya ya utajiri kwa nchi iliyoshuhudia migogoro na umasikini katika Pembe ya Afrika.Baadhi ya raia lakini wamelalamika kuwa pesa zilizotumiwa kwa ujenzi wa ukumbi wa tamasha,zingeweza kutumiwa bora zaidi.